Miaka hamsini mwanzoni, katika kitabu chakeKwanini mimi si mkristu, asiyeamini Mungu Bertrand Russell alishtusha watu wa kizazi chake kwa kuhoji kuwapo kwa Yesu. Aliandika:
“Kihistoria inatia shaka kwamba Kristo alikuwapo hata kidogo, na kama alikuwapo, hatujui kitu chochote kuhusu Yeye, hivyo sihusiki na suala la kihistoria, ambalo ni gumu sana.”[2]
Inawezekana kwamba Yesu wengi wanaomwamini hakuwahi kuwapo? Katika Hadithi ya Ustaarabu, mwanahistoria wa kawaida Will Durant alileta swali hili: “Yesu aliwahi kuwapo? Ni hadithi ya maisha ya mwasisi wa Ukristu, matokeo ya huzuni ya mwanadamu, fikira na matumaini – hadithi inayolingana na ya Krishna, Osiris, Attis, Adonis, Dionysus na Mithras?” [3] Durant alionesha jinsi gani hadithi ya ukristu ina mifanano mingi ya kutia shaka kwa hadithi za miungu ya kipagani.”[4]
Baadaye katika makala hii tutaona jinsi gani huyu mwanahistoria mkubwa alijibu swali lake mwenyewe kuhusu kuwapo kwa Yesu. Kwa hiyo, jinsi gani tunaweza kujua kwa uhakika kwamba mtu huyu, ambaye wengi wanamwabudu na wengine wanamlaani, alikuwapo kweli? Johnson yupo sawa wakati aliposema kwamba Yesu Kristo ni mkusanyiko toka kwa miungu wengine? Na Russell yuko sawa wakati aliposema kwamba kuwapo kwa Yesu ni “mashaka kabisa”?