Habari hizi za kweli zinazofuata kuhusu Yesu ziliandikwa na vyanzo vya kale visivyo vya kikristu:
- Yesu alikuwa wa kutoka Nazareth.
- Yesu aliishi maisha ya busara na maadilifu.
- Yesu alisulubiwa nchini Yuda chini ya Pontio Pilato wakati wa utawala wa Tiberius Caesar wakati wa Pasaka, akidhaniwa kuwa ni Mfalme wa Wayahudi.
- Yesu aliaminiwa na wafuasi wake kuwa amekufa na amefufuka toka katika wafu siku tatu baadaye.
- Maadui wa Yesu walikubali kwamba alitenda mambo yasiyo ya kawaida waliyoiita “miujiza.”
- Kundi ndogo ya wafuasi wa Yesu liliongezeka haraka, likaenea mbali hadi Roma.
- Wafuasi wa Yesu walikataa miungu mingi, waliishi maisha maadilifu, na walimwabudu Kristo kama Mungu.
Mwanateolojia Norman Geisler aliandika:
“Maelezo haya ya jumla yanaendana kikamilifu na hayo ya Agano Jipya”[9]
Yote katika ya haya maelezo yasiyotegemeana, ya kidini na kawaida, yanazungumzia mtu wa kweli aliyelingana sawa na Yesu katika Injili. Encyclopedia Britannica inanukuu haya maenezo mbalimbali ya kawaida ya maisha ya Yesu kuwa ni ushahidi thibitifu wa kuwapo kwake. Inaeleza:
“Maelezo haya yasiyotegemeana yanathibitisha kwamba katika nyakazi za kale hata wapinzani wa Ukristu hawakutilia shaka uwekaji historia ya Yesu.”[10]