Maelezo ya Watu Wasio-Wakristu wa kale
Hivyo wanahistoria gani wa karne ya kwanza walioandika habari ya Yesu hawakuwa na agenda ya kikristu? Kwanza kabla ya yote, hebu tuangalie kwa hao maadui wa Yesu.
Wapinzani wake wa Kiyahudi walikuwa na mengi ya kufaidika kwa kukana kuwapo kwa Yesu. Lakini ushahidi unaonesha katika uelekeo mwingine. “Maandiko kadhaa ya Kiyahudi pia yanaelezea kuwapo kwa mwili na damu yake. Maandiko yote ya Gemara ya Kitabu cha Wayahudi; Talmud yanamtaja Yesu. Ingawaje haya yanajumuisha vifungu vichache vifupi vilivyokusudiwa kutohesabu utakatifu wa Yesu, maandiko haya ya kale ya Kiyahudi hayaanzi kusema kwamba hakuwa mtu wa kihistoria.”[5]
Flavius Josephus alitambulika kama mwanahistoria wa Kiyahudi aliyeanza kuandika chini ya Mamlaka ya Kirumi A.D. 67. Josephus, ambaye alizaliwa miaka michache baada ya Yesu kufa, angefahamu kwa kina zaidi sifa ya Yesu miongoni mwa Warumi na Wayahudi. Katika zile maarufu Nyakati za Wayahudi (A.D. 93), Josephus aliandika habari ya Yesu kuwa ni mtu kweli. “Katika wakati huo Yesu aliishi kama mtu mtakatifu, ikiwa mtu aliweza kupewa sifa hiyo, kwa kuwa alifanya kazi za ajabu, na alifundisha watu, na kwa furaha aliupokea ukweli. Na alifuatwa na wayahudi wengi na wagiriki wengi. Alikuwa ni Masiha.”[6] Ingawa kuna ubishi kuhusu baadhi ya maneno katika maelezo, hasa kumbukumbu kwa Yesu kuwa Masiha (wasomi wanahoji, wanafikiri kwamba wakristu waliingiza vineno hivi (kirai), kwa hakika Josephus alihakikisha kuwapo kwake.
Vipi kuhusu wanahistoria wa kawaida ambao waliishi katika nyakati za kale lakini hawakuchochewa kidini? Kuna uthibitisho uliopo wa waandishi angalau 19 wa kawaida wa kale ambao walitengeneza kumbukumbu za Yesu kuwa ni mtu wa kweli.[7]
Mmoja wa wanahistoria wakubwa kwa nyakati za kale, Cornelius Tacitus, alitangaza kwamba Yesu aliteseka chini ya Pilato. Tacitus alizaliwa karibu miaka 25 baada ya Jesu kufa, na alikwisha ona kuenea kwa Ukristu kukianza kuimeza Roma. Mwanahistoria wa Kirumi aliyeandika kinyume cha Kristo na Wakristo, akiwatambulisha mwaka A.D. 115 kama harakati za watu waliochukizwa kwa matendo yao maovu, na kwa kawaida waliitwa Chrestiani. Jina lilitolewa toka kwa Chretus, ambaye, katika utawala wa Tiberius, aliteswa chini ya Pontius Pilato, Wakili wa Yuda.”[8]