Mkosoaji mmoja ambaye alifikiri Yesu alikuwa mzushi alikuwa mwandishi wa habari wa Uingereza Malcolm Muggeridge. Lakini kwenye kipindi cha Televisheni kwa Israel, Muggeridge alikabiliwa na ushahidi kuhusu Yesu Kristo ambao hakujua ulikuwapo. Wakati akiangalia sehemu za kihistoria – Sehemu aliyozaliwa Yesu ya Bethlehem, mji wa Nazareth, eneo la kusulubishiwa, na kaburi tupu – hisia za Ukweli wa Yesu zilianza kujitokeza.
Baadaye alieleza:
“Ilikuwa ni wakati nilipokuwa katika Ardhi Takatifu kwa dhumuni la kufanya vipindi vitatu vya Televisheni vya BBC katika Agano Jipya kwamba uhalisia ulinishika kuhusu kuzaliwa kwa Yesu, idara yake na kusulubiwa. …Nikafahamu kwamba kulikuwa na mtu, Yesu, ambaye pia alikuwa Mungu.”[15]
Baadhi ya wasomi wajerumani wadadisi zaidi katika karne za 18 na 19 walihoji kuwapo kwa Yesu, wakizungumzia wahusika wakuu kama Pontio Pilato na kasisi mkuu Joseph Caiaphas katika maelezo ya Injili hawajahakikishwa kuwa kweli. Hakuna kanushi zilizowezekana hadi katikati ya karne ya 20.
Mwanaakilojia (mwana-elimu kale) katika mwaka 1962 alihakikisha kuwapo kwa Pilato wakati walipogundua jina lake likiwamo katika maandishi yaliyochongwa katika jiwe lililochimbwa. Vile vile, kuwapo kwa Caiaphas hakukuwa dhahiri hadi 1990, wakati kasha la mifupa lilipogunduliwa likiwa na maandishi yake yaliyochongwa. Wana-elimu kale (wana-akiolojia) pia wamegundua kile wanachoamini kuwa nyumba ya Simoni Petro and pango ambapo Yohana mbatizaji alipofanyia ubatizaji wake.
Mwishowe, labda ushahidi mwingine unaothibitisha zaidi kwamba Yesu alikuwapo ni mwongezeko kwa kasi wa ukristu. Jinsi gani inaweza kuelezwa bila Kristo? Jinsi gani hili kundi la wavuvi and wafanyakazi wengine walimfahamu Yesu ndani ya miaka michache? Durant alijibu swali lake mwenyewe la utangulizi – Yesu alikuwapo? —kwa hitimisho lifuatalo:
Kwamba watu wachache wa kawaida ndani ya kizazi kimoja wangefahamu wasifu wa mtu mwenye nguvu na kuvutia sana, mzito na mwenye maadili na anayeongoza maono ya udugu wa kibinadamu, ni muujiza ajabu zaidi kuliko yote katika Injili . Baada ya karne mbili za Ukosoaji Mkali, maelezo ya maisha, tabia na mafundisho ya Kristo yalibaki wazi kimsingi, na sura ya kupendeza katika historia ya mtu wa magharibi.