Kweli ni historia ya Yesu?
Mwaka 1945 ugunduzi ulifanyika nchini Misri ya Juu, karibu na mji wa Nag Hammadi. Nakala hamsini na mbili za maandiko ya kale, yaliyoitwa Injili za siri yalionekana katika vitabu 13 vya ngozi vilivyoandikwa kwa mkono. Yaliandikwa kwa lugha ya Kikoptiki iliyokuwa maktaba katika Jumba la Utawa.
Wasomi wachache wa maandiko hayo ya siri wameenda mbali kudai kwamba maandiko haya yaliyogunduliwa hivi karibuni ni historia yakini ya Yesu badala ya Agano Jipya. Je, imani yao katika maandiko haya inaendana pamoja na ushahidi wa kihistoria? Hebu tuangalie kwa kina kuona kama tunaweza kutenganisha ukweli kutoka katika kubuni.
“Wajuaji” wa siri
Injili za Siri zinahusishwa katika kikundi kijulikanacho kama (shangazo kubwa hapa) Wajuaji wa siri. Jina lao linatoka katika neno la kigiriki, linamaanisha “maarifa”. Watu hawa walifikiria walikuwa na siri, ufahamu maalumu uliojificha kwa watu wa kawaida.
Kwa kadri ukristo ulivyoenea, Wanostiki (Wajuaji wachache) walichanganya imani baadhi na masuala ya ukristo kwenye imani zao, wakibadili Unostiki (Usiri) kuwa ukristu bandia. Labda walifanya hivyo kuongeza idadi ya washirika na kumfanya Yesu mtoto wa matangazo kwa sababu zao. Vile vile, kwa mfumo wao wa fikra kuendana na ukristu, Yesu alihitaji kuelezewa upya, kuvuliwa yote ubinadamu wake na uungu wake halisi.
Katika historia ya Ukristu ya Oxford, John McManners aliandika mchanganyiko imani za Kinostiki, kikristo na kizushi.
Ujuzi-siri ulikuwa (na bado ni) theosophia (elimu ya Mungu ya kiroho) zenye michanganyiko mingi. Ushirikina na imani za kizushi za kienyeji zilichanganywa na elimu ya nyota, uchawi. … Wakakusanya misemo ya Yesu iliyotengenezwa kufaa tafsiri zao (kama katika Injili ya Thomaso), na wakawapa wafuasi wao fursa au namna ya upinzani wa Ukristu.[1]
« Previous | Next »