Mwili Count
Sisi sote twashangaa kitu gani kitatokea kwetu baada ya sisi kufa. Wakati mpendwa anapokufa, twatamani kumuona tena baada ya zamu yetu kufika. Je, tutakuwa na mjumuiko wa kufurahisha na hao tuwapendao au kifo ni mwisho wa fahamu zote?
Yesu alifundisha kwamba maisha hayakomi baada ya miili yetu kufa. Aliweka dai hili la kupendeza: “Mimi ni ufufuo na uzima. Hao wanaoaamini kwangu, japo wafa kama my yeyote mwingine, wataishi tena” Kulingana na mashahidi wa macho walio karibu zaidi nay eye, Yesu pia alionesha uwezo wake dhidi ya kifo kwa kufufuka toka katika wafu baada ya kusulubiwa and kuzikwa kwa siku tatu. Ni hii imani ambayo imewapa matumaini wakristu kwa karibu miaka 2000.
Lakini baadhi ya watu hawana tumaini la maisha baada ya kifo. Mwanafalsafa wa wasioamini uwapo wa Mungu, Bertrand Russell aliandika, “Ninaamini kwamba wakati nitakapokufa, nitaoza, na hakuna chochote cha nafsi yangu kitaishi” [1] Russell dhahiri hakuamini maneno ya Yesu.
Wafuasi wa Yesu waliandika kwamba alionekana hai kwao baada ya kusulubiwa na kuzikwa. Hawakudai kumuona tu bali pia walikula pamoja naye, walimshika na walimaliza siku 40 wakiwa naye.
Kwa hiyo, hii ingeweza kuwa ni hadithi tu ambayo imekuwapo kwa muda, au inathibitishwa kwa ushahidi mzito? Jibu kwa swali hili ni msingi kwa Ukristo. Kwa sababu ikiwa Yesu alifufuka toka katika wafu, ingehakikisha kila kitu kujihusu yeye, kuhusu maana ya maisha na kuhusu hali zetu baada ya kifo.
Ikiwa Yesu alifufuka toka katika wafu, basi yeye peke yake angekuwa na majibu kwa maisha yalivyo na kitu kinatukabili baada ya kufa. Kwa upande mwingine, ikiwa maelezo ya ufufuko wa Yesu is ya kweli, basi uKristu ungekuwa umeanzishwa kwenye uongo! Mwanateolojia R.C. Sproul anaweka wazi hivi:
“Madai ya ufufuko ni muhimu kwa Ukristo. Ikiwa Kristo amenyanyuliwa toka katika wafu na Mungu, basi ana mamlaka na uthibitisho kwamba hakuna kiongozi mwingine wa dini anao. Buddha amekufa. Muhammad amekufa. Musa amekufa. Confushazi amekufa. Lakini kwa Ukristo, Kristo yu hai.”[2]
Wakosoaji wengi wamejaribu kupinga ufufuko. Josh McDowell alikuwa ni mmoja wa hao wakosoaji ambaye alitumia zaidi ya saa mia moja akitafiti ushahidi wa ufufuko. McDowell alielezea haya kuhusu umuhimu wa ufufuka.
“Nimefikia hitimisho kwamba aidha ufufuko wa Yesu Kristo ni udanganyifu mbaya usiojali uliowahi kuwekwa katika akili za watu, au ni ukweli mkuu wa ajabu wa historia.”[3]
Kwa hiyo, je ufufuko wa Yesu ni ukweli au hadithi za kutunga? Kujua, twahitaji kuangalia ushahidi wa historia na kufanya hitimisho zetu. Ngoja tuangalie kile wakosoaji waliochunguza ufufuko walichogundua wao wenyewe.
« Previous | Next »