Yesu na Maria Magdalena:
Walikuwa na ndoa ya siri?
Misezi Yesu
Je, historia imekuwa sio sahihi kwa miaka 2000—kulikuwa na Mrs. Yesu Kristo? In, “Kaburi la Familia ya Yesu,” mkurugenzi wa (makala ya Chaneli ya TV ya Discovery) Simcha Jacobovici anadai kuna “ushahidi” kwamba Yesu na Maria Magdalena walioana na walikuwa na mtoto aliyeitwa Yuda.
(Kuona kitu gani wasomi wanasema kuhusu “ushahidi” wa Jacobovici angalia, saa Wasifu Uliozaliwa.)
Jacobovici si mtu wa kwanza kudai uhusiano wa kimapenzi unaowezekana kati ya Yesu na Maria . Sinema, Jaribio la Mwisho la Kristo, na vitabu kama Damu Takatifu, Kikombe Kitakatifu, na maandishi ya Da Vinci, yalifanya siri uhusiano kati ya Yesu na Maria kuwa sehemu kuu ya habari zao.
Maandishi ya Da Vinci yanaanza na ukurasa wa ukweli ambao unafanya hadithi ya kutunga kuonekana kuwa kweli katika madai yake yote. Kitabu kimevunja rekodi zote katika orodha ya mauzo bora ya New York, na imefuatiwa na sinema fanikifu kibiashara. Ukusanya hodari wa ukweli wa mtunzi Dan Brown pamoja na ubunifu umewaaminisha wasomaji wengi kwamba Yesu na Maria Magdalena walikuwa wameoana na walikuwa na mtoto (Angalia saa Tabasamu la MonaLisa). Lakini madai haya ya kimapenzi yanatangaza sana vitabu na sinema, au yanaungwa mkono na ushahidi wa kihistoria.
Maria wa Siri
Kabla hatujachunguza ushahidi kwa mapenzi yoyote yanayowezekana kati ya Yesu na Maria Magdalena, tuangalie mtu huyu Maria kutoka mji mdogo wa Galilaya wa Magdala. Kwa kuanza tunauliza swali, ni maandiko gani ya kale yanatoa mwanga kwa tabia yake na uhusiano wake na Yesu wa Nazareth?
Injili za Agano Jipya ni rekodi za zamani za Maria wa Magdala. Katika Injili Maria anaelezewa kama mwanamke ambaye Yesu alimponya kumilikiwa na mashetani. Injili (Mathayo, Marko, Luka na Yohana) zinamwelezea Maria kama mfuasi wa Yesu ambaye alisikiliza mafundisho yake, alitoa mahitaji yake ya kifedha, alishuhudia kusulubiwa kwake, na siku tatu baadaye alikuwa wa kwanza kumuona hai.
Baadhi wamesema Maria Magdalena alikuwa malaya, lakini si mitume wala kanisa la kale wamemzungumzia zaidi ya kusema alikuwa mmoja wa wafuasi wa karibu wa Yesu. Wazo kwamba alikuwa malaya lilianza karne ya sita, wakati Papa Gregory wa Kwanza alipomtambua yeye kama mwanamke aliyezungumziwa katika Luka 7:37, na mwanamke aliyeosha miguu ya Yesu kwa nywele zake.
Ingawaje maoni ya Papa yawezekana yalisababishwa na ukweli kwamba Yesu alipunga mapepo saba kutoka kwake, hakuna msomi wa Biblia anaweza kufanya mhusisho kuhusu Mary Magdalena na mwanamke katika vifungu vya Luka. Kwa nyongeza, Injili za Agano Jipya hazidokezi kitu chochote kile cha kimapenzi kati ya Yesu na Maria.
Hivyo wapi wananadharia wa hila wanapata wazo? Kwanini madai haya yote? Kwa hilo tunageukia maandiko yaliyoandikwa miaka 100 – 200 baada ya Injili za Agano Jipya na dhehebu lisilo la kikristu lililoitwa Wanostiki (Wazushi/Wajuaji wachache) (Angalia saa Injili Za Siri) Maandiko haya si sehemu ya Agano Jipya, na yalikataliwa na wakristu wa kale kuwa ni ya kizushi na yako kinyume. Hao wanaoandika uhusiano wa kimapenzi katia ya Yesu na Maria wananukuu vifungu vichache kutoka maandiko mawili ya maandiko hayo, Injili ya Maria na Injili ya Philipo. Tuangalie katika vifungu hivyo.
« Previous | Next »