Yesu ni nani Halisi?

Ukweli kuhusu Yesu Kristo.

  • Kiingereza Home
  • Swahili Home
  • Kutuma Maoni

Yesu Alikuwa mtu Kweli?

Wasifu Uliozaliwa

Yesu Kristo kweli alikuwapo, au Ukristu umejengwa kwa uzushi? Wasomi wachache wanahoji kuwapo kwa Yesu, lakini baadhi ya maadui wa ukristu wanajaribu kuthibitisha vinginevyo.

Katika shitaka dhidi ya Vatican, Kanisa lilishitakiwa kwa kubuni uzushi wa  kuwapo kwa Yesu. Ingawaje kesi ilitupiliwa nje ya Mahakama mwezi Februari 2006, mdai, Luigi Cascioli, alikata rufaa, lakini mwishowe kesi yake ilifungwa.

Madai dhidi ya uwapo wa Yesu yaliwekwa wazi kwenye Televisheni ya CNN wakati Ellen Johnson, raisi wa wasioamini kuwapo kwa Mungu wa Marekani, walipotangaza:

“Ukweli ni kwamba hakuna hata chembe ya ushahidi wa kawaida kuwa kulikuwapo na Yesu Kristo. Yesu Kristo na Ukristu ni dini ya siku hizi. Na Yesu Kristo ni mkusanyo toka miungu mingine: Osiris, Mithras, aliyekuwa na asili ile ile, kifo kile kile kama cha kiimani cha Yesu Kristo.” Ellen Johnson, mpagani

Johnson na baraza la utepe-bluu la viongozi wa kidini walikuwa wakijadili swali, “Kitu gani kinatokea baada sisi kufa?” kwenye kipindi cha moja kwa moja cha Larry King Live katika matangazo ya CNN. Mtangazaji King aliyetulia mara nyingi aliketi kwa makini na kisha akajibu.”Kwa hiyo hauamini kulikuwa na Yesu Kristo?

Kwa hali ya uhakika, Johnson alijibu, “Hakuwapo.” Si kile ninachoamini; hakuna ushahidi wa kawaida kwamba YK, Yesu Kristo alikuwapo.”

King hakufuatilia na alienda katizoni kwa Tangazo la Biashara. Hakuna mjadala wa ushahidi wowote kwa ajili au dhidi ya kuwapo kwa Yesu ulikuwa unakuja. Watazamaji wa kimataifa wa Televisheni waliachwa wakishangaa.[1]

« Previous | Next »

Pages: 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10

Yesu ni nani Halisi?

  • Yesu Alikuwa mtu Kweli?
  • Kulikuwa na Hila za Da Vinci?
  • Yesu ni Mungu?
  • Injili ni za Kweli?
  • Yesu Alikuwa Masiha?
  • Je, Yesu Alifufuka toka Katika Wafu?
  • Yesu ni Muhimu Leo?

MASWALI ZAIDI KUHUSU YESU

  • Yesu na Maria Magdalena: Walikuwa na ndoa ya siri?
  • Injili za Siri: Kuna maandiko ya siri kuhusu Yesu?
Copyright © 2025 - JesusOnline
Menu
  • Yesu Alikuwa mtu Kweli?
  • Kulikuwa na Hila za Da Vinci?
  • Yesu ni Mungu?
  • Injili ni za Kweli?
  • Yesu Alikuwa Masiha?
  • Je, Yesu Alifufuka toka Katika Wafu?
  • Yesu ni Muhimu Leo?
  • Yesu na Maria Magdalena: Walikuwa na ndoa ya siri?
  • Injili za Siri: Kuna maandiko ya siri kuhusu Yesu?