Njia Ya Mitume
Ushahidi gani upo kwamba Yesu ni yule ambaye kweli alidai kuwa? Jinsi gani tunajua, hakuwa aina fulani ya mbabaishaji feki? Hebu tuangalie baadhi ya wababaishaji feki maarufu na tuone iwapo sifa hiyo inamfaa Yesu, au kwamba kuna ushahidi kuunga mkono madai yake.
Ferdinand Waldo Demara, mdogo, aliitwa mbabaishaji feki mkubwa. Demara alikuwa na utambulisho feki bandia wa mwanasaikolojia, mhadhiri wa chuo kikuu, mkuu wa idara ya chuo, na mkuu wa gereza. Alifanya hata upasuaji, akiwa kama daktari bogasi feki.
Baadhi wanadai kwamba Frank Abagnale alikuwa pia mbabaishaji feki mkubwa. Kati ya miaka 16 na 21, Abagnale alikuwa ni mmoja wa wasanii matapeli wenye mafanikio zaidi duniani. Aliwakabidhi cheki bandia za dola milioni mbili na nusu (2.5) katika nchi zote 50 na nchi 26 za kigeni.. Pia alifanikiwa kujifaulisha mwenyewe kama rubani wa ndege, mwanasheria, profesa wa chuo na mtaalamu wa magonjwa ya watoto kabla hajakamatwa na Polisi wa Ufaransa..
Ikiwa hadithi hii inaonekana kufahamika kwako, inawezekana ni kwa sababu ulitazama sinema ya mwaka 2002 Nikamate Kama Unaweza, ambamo Abagnale aliigizwa na Leonardo DiCaprio (ambaye alijipasisha mwenyewe kama mwingizaji katika Titanic).
Kitu gani kingefaa kushinda uigizaji wa Abagnale kama mtu tapeli? Haya, ikiwa Yesu Kristo hakuwa Masiha aliyedai kuwa, kungekuwa hakuna shindano. Hatuzungumzii kuhusu maelfu ya wanaotapeli, kama katika kesi ya Abagnale. Ikiwa Yesu Kristo alikuwa tapeli mbabaishaji feki, kazi yake ya utapeli ilidanganya mabilioni ya watu na ilibadilisha mwenendo wa miaka 2000 ya historia.
Hivyo Yesu angeweza kuwa Masiha feki, akidanganya hata wasomi wa kidini wakubwa? Inawezekana aliandaliwa na wazazi wake au wakufunzi wasiojulikana ili kuwa mfalme aliyeahidiwa muda mrefu ambaye Israel ilikuwa inamtafuta?
Kwa kweli, ikiwa Yesu alikuwa mbabaishaji feki, asingekuwa mtu wa kwanza katika historia ya Israel kuwa amedanganya kuhusu kuwa Masiha. Kupita karne zote kabla ya kuzaliwa Kristo, na baadaye pia, masiha wengi waliojitangaza wenyewe walitokea kuonekana kama matapeli na wendawazimu.
Tabiri za waebrania wa kale zilitabiri wazi utawala wa mfalme ajaye ambaye angeleta amani kwa Israel na kuwa mkombozi wao. Hali ya matarajio yaliijaza nchi na yalishika matumaini na matarajio ya wayahudi. Katika mazingira hayo kama ya waisraeli, ingewezekana mtu ambaye ana sifa kidogo, awekwe, au ajifananishe mwenyewe kufaa umbile la Masiha? Jibu kwa swali hilo limebaki katika Tabiri za Agano la Kale zikimwonyesha Masiha.
« Previous | Next »