Hadithi dhidi ya Ukweli
Ngoja tuanze na swali la msingi zaidi: Kitu gani kinatofautisha hadithi na ukweli? Jinsi gani tunajua, kwa mfano, kwamba Alexander Mkuu alikuwapo kweli? Inavyoaminika, katika mwaka 336 baada ya Kristo, Alexander Mkuu alikuwa mfalme wa Masedonia katika umri wa miaka 20.. Mwerevu wa jeshi, huyu kiongozi maridadi mwenye kiburi alichanja njia kupitia vijiji, miji na falme za Uajemi za Greco hadi akazitawala zote. Katika kipindi kifupi cha miaka minane majeshi ya Alexander yalivuka jumla ya maili 22,000 katika kuzishinda kwake na kuzitwaa nchi hizo.
Imekuwa ikisemwa kuwa Alexander alikuwa akilia wakati alipozikimbilia nchi za kuzishinda. (Ninafikiri huyu siye mtu ninayetaka kucheza naye.)
Kabla hajafa katika umri wa miaka 32, Alexander inavyoripotiwa alitimiza vitendo vikubwa vya jeshi kuliko yeyote katika historia, sio tu za wafalme walioishi kabla yake, lakini pia vya hao waliokuja baadaye, hadi katika wakati wetu. Lakini leo, mingineyo ya idadi ya miji iliyoitwa Alexandria, sinema inayochosha na Oliver Stone, na vitabu vichache, urithi wake wote umesahaulika. Kwa kweli jina Colin Farrell lina nguvu zaidi ya kuvutia katika ofisi ya sinema kuliko jina la Alexander.
Licha ya kushindwa kwa ofisi ya sinema, wanahistoria wanaamini Alexander alikuwapo kwa sababu ya sababu tatu za msingi:
- Nyaraka zilizoandikwa kutoka kwa wanahistoria wa zamani.
- Mchango wa kihistoria.
- Ushahidi wa kihistoria na kitafiti.
Nyaraka za Kihistoria Kuhusu Yesu
Historia ya Alexander Mkubwa na ushindi wake wa kijeshi unapatikana kutoka katika vyanzo vitano vya kale, hakuna hata kimojawapo kilikuwa na mashahidi wa macho. Ingawaje imeandikwa miaka 400 baada ya Alexander, Kitabu cha Plutarch Cha Maisha ya Alexander ni maelezo ya msingi ya maisha yake.
Kwa Bw. Plutarch and waandishi wengine waliondolewa miaka mia saba kutoka katika matukio ya maisha ya Alexander, walitegemeza taarifa zao katika maelezo ya mwanzo. Kati ya maelezo ishirini ya kihistoria ya wakati huo kuhusu Alexander, hakuna hata mojawapo linaendelea kuwapo. Maelezo ya baadaye yapo, lakini kila moja linamwelezea “Alexander” tofauti, kabisa na kufikiria kwetu. Lakini bila kujali pengo la muda la miaka saba, wanahistoria wanaaminishwa kwamba Alexander alikuwa ni mtu wa kweli na kwamba maelezo ya msingi ya kile tusomacho kuhusu maisha yake ni kweli.
Tukimweka Alexander kama hoja ya kukumbushia, tutatambua kwamba kwa Yesu kuna maelezo yote ya kidini na ya kihistoria ya kawaida. Lakini lazima tuulize swali, yaliandikwa na wanahistoria wa kuaminika wenye mwelekeo? Hebu tuangalie kwa kifupi.