Agano Jipya
Vitabu 27 vya Agano Jipya vinadaiwa kuandikwa na watunzi ambao aidha walimjua Yesu au walipokea ufahamu wake wa kwanza toka kwa wengine. Maelezo ya Injili nne zinarekodi maisha na maneno ya Yesu kutoka katika mitazamo tofauti. Maelezo haya yamechunguzwa kwa makini sana na wasomi wote wa Ukristu na nje yake.
Msomi John Dominic Crossan anaamini kwamba chini ya asimilia 20 ya kile tusomacho katika Injili ni maneno halisi ya Yesu. Hata huyu mkosoaji habishi kwamba Yesu Kristo kweli aliishi.
Licha ya maoni ya Crossan, na wale wasomi wachache wa upande mwingine kama Yeye, makubaliano ya wanahistoria wengi ni kwamba maelezo ya Injili yanatupa sisi picha nzuri ya Yesu Kristo. Iwe kwamba maelezo ya Agano Jipya ni ya kuaminiwa ni somo la makala nyingine (Angalia “Andiko la Yesu”), hivyo tutaangalia kwenye vyanzo vingine visivyo vya kikristu kwa jibu letu kwamba Yesu alikuwapo.