Andiko la Yesu
Injili za Agano Jipya ni ushahidi wa macho wa kweli wa historia ya Yesu Kristo, au ni hadithi zimebadilishwa kwa miaka mingi? Lazime tuchukue maelezo ya Agano Jipya ya Yesu kwa imani, au kuna ushahidi kwa uhakika wake?
Marehemu Mratibu wa Habari za ABC, Peter Jennings alikuwa nchini Israeli akitanganza kipindi cha televisheni maalumu kwa Yesu Kristo. Kipindi chake, kiitwacho “Kumtafuta Yesu,” alichunguza swali la kwamba Yesu wa Agano Jipya alikuwa sahihi kihistoria.
Jennings alichukua maoni katika maelezo ya Injili toka kwa De Paul, profesa John Dominic Crossan, watatu kati ya wanachuo-wenza wa Crossan toka katika Semina ya Yesu, na wasomi wengine wawili wa Biblia. (Semina ya Yesu ni kikundi cha wasomi wanaojadili maneno na matendo ya Yesu yaliyorekodiwa na kisha wanatumia vishanga vyekundu, pinki, kijivu au vyeusi kupiga kura kuonesha jinsi gani kiaminifu wanaamini maelezo katika Injili yalivyo.)[1]
Baadhi ya maoni yalikuwa yakishangaza. Pale kwenye TV ya Taifa Dk. Crossan sio tu alionesha shaka kwa zaidi ya asilimia 80 ya maneno ya Yesu lakini pia aliyakana madai ya Yesu ya utakatifu, miujiza yake, na kufufuka kwake. Jennings waziwazi alivutiwa na taswira ya Yesu ilivyowasilishwa na Crossan.
Kutafuta historia ya kweli ya Biblia siku zote ni habari, ambayo ndio maana kila mwaka gazeti la Time na Newsweek linaendelea kuandika simulizi kwenye ukurasa wa mbele kwa ajili ya Maria, Yesu, Musa au Abraham. Au—nani anajua? —labda mwaka huu itakuwa “Bob: Simulizi ambayo haijasimulizwa ya Mfuasi wa 13 anayekosekana.”
Hii ni burudani, na hivyo uchunguzi hautaisha wala kutoa majibu, kwa sababu kufanya hivyo kutamaliza hata kukosesha vipindi vya wakati ujao. Badala yake, hao wenye maoni tofauti sana wanatupwa pamoja kama mwendelezo wa shujaa bila matumaini achanganyaye jambo kuliko kuleta ukweli.
Lakini ripoti ya Jennings ililenga kwenye suala moja ambalo linatakiwa kupewa ufikiriaji wa dhati. Crossan alidokeza kwamba maelezo halisi ya Yesu yalikolezwa na simulizi za jadi na hayakuandikwa hadi baada ya mitume walipokuwa wamekufa. Hivyo kwa kiasi kikubwa hayaaminiki na yanashindwa kutupa sisi picha sahihi ya Yesu wa kweli. Jinsi gani tunapaswa kujua ikiwa hii ni kweli kabisa?
« Previous | Next »