Mchango wa kihistoria
Tofauti muhimu kati ya uzushi na mtu wa kweli ni jinsi gani mtu anavyobadili historia. Kwa mfano, vitabu vimeandikwa na sinema zimetengenezwa kuhusu Mfalme Arthur wa Camelot na mashujaa wake wa meza ya duara. Wahusika hawa wamekuwa mahiri kiasi wengi wanaamini walikuwa watu kweli. Lakini wanahistoria wametafuta vyanzo kwa kuwapo kwao wameshindwa kugundua faida yoyote waliyo nayo kwenye sheria, maadili au dini. Himaya pamoja na ukuu wa Camelot kwa hakika ungeacha alama zake kwenye historia za wakati huo. Kukosekana huku kwa umuhimu wa kihistoria kunaonesha Mfalme Arthur na mashujaa wake wa meza ya duara ni wa kutunga tu.
Mwanahistoria Thomas Carlyle alisema, “Hakuna mtu mkuu anayeishi bure. Historia ya dunia ni habari ya watu wakuu.”[11] Kama Carlyle alivyonoti, ni watu wa kweli, sio hadithi, ambayo wanabadili historia.
Akiwa mtu kweli, Alexander alibadili historia kwa ushindi wa majeshi yake, alibadili mataifa, serikali na sheria. Lakini vipi kuhusu Kristo na mchango wake katika dunia yetu?
Serikali za karne ya kwanza za Yuda and Roma hazikuguswa kwa kiasi kikubwa na maisha ya Yesu. Mwananchi wa kawaida wa Rumi hakujua alikuwapo hadi miaka mingi baada ya kifo chake. Utamaduni wa kirumi ulibaki kwa kiasi kikubwa kimya na mbali na mafundisho yake kwa miongo kadhaa, na ingeweza kuwa karne kadhaa kabla ya kuua wakristu katika uwanja wa mauaji hakujawa starehe ya kupotezea muda ya kitaifa. Sehemu ya dunia iliyobaki ilikuwa nazo kidogo kama zilikuwapo taarifa zake. Yesu hakukusanya jeshi. Hakuandika kitabu wala kubadilisha sheria. Viongozi wa kiyahudi walitarajia kufuta kumbukumbu zake na ilionekana wangefanikiwa.
Leo, hata hivyo, Roma ya kale imelala katika magofu. Majeshi yenye nguvu ya Kaizari mfahari wa mamlaka ya kibeberu ya Rumi yamepotelea katika kusahauliwa. Lakini jinsi gani Yesu anakumbukwa leo? Ni nini huo wake mvuto unaoendelea?
- Vitabu vingi vimeandikiwa kuhusu Yesu kuliko mtu mwingine yeyote katika historia.
- Mataifa yametumia maneno yake kama kanuni za msingi katika serikali zao. Kulingana na Durant, “Shangwe ya Kristo ilikuwa ndio mwanzo ya demokrasia.”[12]
- Mafundisho yake katika mlima yaliweka mfano halisi mpya katika kanuni na maadili.
- Shule, hospitali na kazi za kibinadamu zimeanzishwa kwa jina lake. Harvard, Yale, Princeton, na Oxford ni vyuo vichache ambavyo vina wakristo wa kuwashukuru kwa kuanzishwa kwao.
- Faida zilizoheshimiwa za wanawake katika Utamaduni wa Magharibi zinaelekezea mizizi yake kwa Yesu. (Wanawake katika nyakati za Yesu walifikiriwa kuwa duni na si watu hadi mafundisho yake yalipofuatwa.)
- Utumwa ulikomeshwa nchini Uingereza na Marekani kutokana na mafundisho ya Yesu kwamba kila maisha ya binadamu yana thamani kuthaminika.
- Wategemezi wa zamani wa madawa ya kulevya na pombe, malaya na wengine watafutao maana katika maisha wanadai yeye kama kielelezo kwa ajili ya maisha yao yaliyobadilika.
- Watu bilioni mbili wanajiita wakristu. Wakati baadhi ni wakristu kwa jina tu, wengine wanaendelea kubadili utamaduni wetu kwa kufundisha maadili ya Yesu kwamba maisha yote ni yenye thamani ya kuthaminika na tunapaswa kupendana, kumpenda kila mmoja.