Yesu ni nani Halisi?

Ukweli kuhusu Yesu Kristo.

  • Kiingereza Home
  • Swahili Home
  • Kutuma Maoni

Yesu Alikuwa mtu Kweli?

Kwa kushangaza, Yesu alifanya yote ya badiliko hili kama matokeo ya idara ya kazi ya kipindi cha miaka mitatu tu. Ikiwa Yesu hakuwapo, mtu lazima ashangae jinsi gani uzushi ungeweza kubadili historia hivyo. Wakati mwanahistoria wa dunia H.G. Wells alipoulizwa nani ameacha urithi mkubwa katika historia, alijibu, “kwa swali hili Yesu anashikilia nafasi ya kwanza.”[13]

Ushahidi wa kimaandishi na faida ya kihistoria unalenga kwenye ukweli kwamba Yesu alikuwapo. Ikiwa Yesu kweli alikuwapo, pia tungetarajia kugundua nyayo zake zilizowekwa ndani ya maelezo yake ya historia. Uzushi, huwa hauachi maelezo ya kuthibitisha hivi.

Moja ya siri hapa kwa Durant na wasomi wengine ni suala la muda. Uzushi na uvumi/hekaya kwa kawaida huchukua mamia ya miaka kuzuka – hadithi ya George Washington hakuwahi kusema uongo inawezekana ilikuwa uongo, hadi karne mbili zilipoibadili kuwa historia. Habari za Ukristu, kwa upande mwingine, zilienea kwa haraka kiasi cha kuhesabiwa kuwa uzushi. Ikiwa Yesu hakuishi, hao ambao wanapinga ukristu wangemwita mzushi tokea mwanzo. Lakini hawakuthubutu.

Ushahidi wa hivyo, sambamba na maelezo yaliondikiwa ya kale na mchango wa kihistoria wa Yesu Kristo, unawaaminisha hata wanahistoria wakosoaji kwamba mwasisi wa Ukristu hakuwa mzushi wala uvumi/hekaya. Lakini mtaalamu mmoja katika uzushi hakuwa na uhakika sana.

Kama Muggeridge, msomi wa Oxford C. S. Lewis mwanzo aliamini kwamba Yesu hakuwa kitu chochote zaidi ya kuwa mzushi. Lewis mwanzo alisema, “Dini zote, yaani imani zote… ni ubunifu tu mwanadamu mwenyewe – Kristo kama ilivyo sana kwa Loki.”[14] (Loki mungu za wa zamani wa Unorweini (Norway). Kama Thor, lakini bila mtindo wa nywele kuzifunga kwa nyuma.)

Miaka kumi baada ya kumkana Yesu kuwa ni uzushi, Lewis aligundua kwamba maelezo ya kihistoria, zikiwamo nyaraka kadhaa za mashahidi wa macho, zinathibitisha kuwapo kwake.

Yesu Kristo ameibadili sura ya historia kama tememeko kubwa la ardhi. Na tetemeko hili limeacha alama ya njia pana kuliko bonde kubwa. Ni alama-njia hii ya ushahidi ambao inawaaminisha wasomi kwamba Yesu kweli alikuwapo na kweli alibadili dunia yetu miaka 2000 iliyopita.

« Previous | Next »

Pages: 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10

Yesu ni nani Halisi?

  • Yesu Alikuwa mtu Kweli?
  • Kulikuwa na Hila za Da Vinci?
  • Yesu ni Mungu?
  • Injili ni za Kweli?
  • Yesu Alikuwa Masiha?
  • Je, Yesu Alifufuka toka Katika Wafu?
  • Yesu ni Muhimu Leo?

MASWALI ZAIDI KUHUSU YESU

  • Yesu na Maria Magdalena: Walikuwa na ndoa ya siri?
  • Injili za Siri: Kuna maandiko ya siri kuhusu Yesu?
Copyright © 2023 - JesusOnline
Menu
  • Yesu Alikuwa mtu Kweli?
  • Kulikuwa na Hila za Da Vinci?
  • Yesu ni Mungu?
  • Injili ni za Kweli?
  • Yesu Alikuwa Masiha?
  • Je, Yesu Alifufuka toka Katika Wafu?
  • Yesu ni Muhimu Leo?
  • Yesu na Maria Magdalena: Walikuwa na ndoa ya siri?
  • Injili za Siri: Kuna maandiko ya siri kuhusu Yesu?