Kipimo cha ndani cha Ushahidi
Kama wapelelezi wazuri wazuri walivyo, wanahistoria wanathibitisha uhakiki kwa kuangalia katika ushahidi wa ndani. Taarifa hizi za ushahidi wa ndani zinadhihirisha motisha za waandishi na utayari wao kuonesha maelezo na sehemu zingine ambazo zingeweza kuthibitishwa. Taarifa za ndani za msingi wasomi hawa wanazotumia kupima uhakika ni zifuatazo:
- Mfuatano ule ule wa ripoti za mashahidi
- maelezo ya majina, sehemu na matukio
- Barua kwa watu binafsi na vikundi vidogo
- sehemu zinazowasumbua waandishi.
- Kuwapo kwa mambo yasiyohusiana yaliyo kinyume
- Kukosekana kwa mambo husika[14]
Hebu tuchukue kama mfano, sinema ya Taa za Usiku wa Ijumaa. Inaonekana kuwa imejikita katika matukio ya kihistoria, lakini kama zilivyo sinema nyingi ambazo kidogo zimejikita katika matukio ya ukweli, inakuacha muda wote ukijiuliza, “Mambo kweli yalitokea hivyo?” Hivyo jinsi gani ungethibitisha uhakika wake wa kihistoria?
Siri moja ingekuwa ni kuwapo kwa mambo yasiyohusiana. Tuseme kwamba katikati ya sinema, mwongozaji, bila sababu maalumu, anapokea simu ikimtaarifu kwamba mama yake na kansa ya ubongo. Jambo hilo halihuani na mtiririko wa sinema na halitajwi tena. Maelezo pekee kwa kuwapo kwa jambo hili lisilohusiana ingekuwa ni kwamba ni kweli lilitokea na kwamba mwongozaji alikuwa na haja ya kuwa sahihi kihistoria.
Mfano mwingine, sinema hiyo hiyo. Tukifuata mtiririko wa mambo, tunataka kikundi cha Permian Panthers (Chui weusi) kushinda ubingwa wa kiTaifa. Lakini hawashindi. Hii ni kinyume na mambo, na haraka tunajua jambo hili lipo pale kwa sababu katika maisha ya kweli, Permian walipoteza mechi ya mchezo. Kuwapo kwa mambo yasiyopendeza pia ni ushahidi wa usahihi wa historia.
Mwisho, matumizi ya miji ya kweli na sehemu zinazojulikana kama Houstone Astrodome zinatuongoza kuchukulia kama ni historia ya vitu hivyo vya hadithi, kwa sababu ni rahisi kuthibitisha au kukanusha.
Hii ni mifano japo ni michache ya jinsi ushahidi wa ndani unatuongoza aidha kuelekea karibu au mbali na hitimisho kwamba andiko fulani linaaminika kihistoria. Tutaangalia kwa kifupi ushahidi wa ndani kwa uhakiki historia ya Agano Jipya.