Ugunduzi wa Codex Sinaiticus
Mwaka 1844 msomi wa Kijerumani Constantine Tischendorf alikuwa akitafuta maandiko ya Agano Jipya. Kwa bahati, aliona kikapu kimejazwa kurasa za zamani katika maktaba ya Jumba la Watawa la Mt. Katherini katika Mlima Sinai. Msomi Mjerumani alifurahishwa japo alishtushwa. Hakuwahi kuona maandiko ya Kigiriki makuukuu hivyo. Tischendorf akamwuliza mkutubi kuhusu karatasi zile na aliogopeshwa sana kufahamu karatasi hizo zilitupwa ili zitumike kama viwashio vya moto. Lundo la Vikapu viwili vya karatasi hizo zilishachomwa tayari!
Shauku ya Tischendorf iliwafanya watawa wawe na wasiwasi, na hawakumwonyesha maandiko mengine zaidi. Hata hivyo, walimruhusu Tischendorf kuchukua kurasa 43 alizogundua.
Miaka kumi na tano baadaye, Tischendorf alirudi katika Jumba la Utawa la Sinai, kipindi hiki pamoja na msaada wa Mrusi Tsar Alexander II. Mara alipokuwa pale, mtawa alimchukua Tischendorf kwenye chumba chake na akavuta kitambaa chenye maandishi ambacho kilikuwa kimehifadhiwa kwenye shefu pamoja na vikapu na sinia. Tischendorf haraka alitambua thamani ya sehemu zilizobaki za maandishi aliyoyaona mwanzoni.
Jumba la Watawa (Monasteri) likakubali kuonesha maandiko kwa Mkuu wa Russia, mlinzi wa Kanisa la Kigiriki. Mwaka 1933 Muungano wa Kisovieti uliuza maandiko kwa Jumba la Makumbusho la Uingereza kwa paundi £100,000.
Codex Sinaiticus ni mojawapo ya maandiko kamili ya zamani ya Agano Jipya tuliyo nayo, na ni miongoni ya zilizo muhimu sana. Baadhi wanakisia kwamba ni mojawapo ya Biblia 50 ambazo mtawala Constantine alimwidhinisha Eusebius kuziandaa mapema karne ya nne. Codex Sinaiticus imekuwa ya msaada mkubwa kwa wasomi katika kuthibitisha na kupima usahihi wa Agano Jipya.