Sura kadhaa za Agano Jipya zinatusaidia kuhakikisha uhakika wake tukiwa tumezingatia yaliyomo na ubora.
Mlolongo
Maandiko bandia aidha huacha ripoti za mashahidi wa macho au haziendani. Kwa hiyo mkinzano wa waziwazi miongoni mwa Injili ungethibitisha kuna makosa. Lakini kwa wakati ule ule, ikiwa kila Injili ilisema kitu kile kile kwa usahihi, ingetia shaka ya kuwapo kushirikiana. Ingekuwa kama vile wala-njama wanajaribu kukubaliana kwa kila elezo la mpango wao. Uwiano uliopita kiasi unatia shaka kama ulivyo uwiano kidogo wa mlolongo.
Mashahidi wa macho kwenye uhalifu au ajali kwa ujumla huelewa tukio kwa usahihi lakini huliona kwa mitazamo tofauti. Vile vile, Injili nne zinaeleza matukio ya maisha ya Yesu kwa mitazamo mbalimbali. Lakini, bila kujali mitazamo, wasomi wa Biblia wanashangazwa na mlolongo wa mtiririko wa maelezo yao na picha nzuri ya Yesu na mafundisho yake, wanavyoyaweka pamoja na ripoti zao za nyongeza.
Maelezo
Wanahistoria wanapenda maelezo ya kina katika maandiko kwa sababu yanafanya iwe rahisi kuthibitisha uhakika. Waraka wa Paulo umejaa maelezo ya kina. Na Injili zimejaa zikiungana nayo. Kwa mfano, vyote Injili za Luka na kitabu chake cha Matendo viliandikwa kwa Bwana mmoja aitwaye Theophilus, ambaye bila shaka alijulikana vizuri wakati huo.
Ikiwa haya maandiko yangekuwa ni uzushi wa mitume, majina bandia, sehemu bandia na matukio bandia yangeonekana kivyepesi na maadui zao, hasa viongozi wa Kiyahudi na Kirumi. Hii ingekuwa ni kama kashifa ya Watergate kwa karne ya kwanza. Lakini mengi ya maelezo ya Agano Jipya yamethibitishwa kuwa kweli kwa uhakiki mbalimbali. Mwanahistoria maarufu wa elimu na lugha, Colin Hermer, kwa mfano,
“anatambua habari 84 za ukweli katika sura 16 za mwisho za Matendo ya Mitume kwamba zimethibitishwa kwa utafiti wa Elimu-kale, akiolojia.” [15]
Katika karne chache zilizotangulia, wasomi wadadisi wa Biblia walishambulia vyote uandishi wa Luka na tarehe zake, wakidai kwamba iliandikwa karne ya pili na mwandishi asiyejulikana. Mwana-elimukale ya akiolojia Bwana William Ramsey aliaminishwa kwamba walikuwa sahihi, na alianza kuchunguza. Baada ya utafiti wa kina, mwanaakiolojia alibadili maoni yake. Ramsey akakubali,
“Luka ni mwanahistoria wa daraja la kwanza. Mwandishi huyu awekwe miongoni mwa wanahistoria wakubwa sana. Historia ya Luka haipitwi kwa heshima na uaminifu wake.”[16]
Maelezo ya Matendo, kazi ya kimisionari ya Paulo, akiorodesha sehemu alizotembelea, watu aliowaona, meseji alizopeleka, na mateso aliyoyapata. Ingewezekana maelezo haya kuwa yameghushiwa? Mwanahistoria wa kirumi A.N. Sherwin-White aliandika,
“Katika Matendo, uhakika wa historia ni mwingi sana kupindukia. Majaribio yoyote kukataa uhakika wake wa historia wa kimsingi kwa sasa lazima uwe ni upuuzi. Wanahistoria wa kirumi wameuchukulia kweli.”[17]
Kuanzia kwenye maelezo ya Injili hadi nyaraka za Paulo, waandishi wa Agano Jipya kwa waziwazi wameelezea maelezo hata kutaja majina wa wahusika ambao walikuwa hai wakati huo. Wanahistoria wamethibitisha angalau majina thelathini kati ya haya.[18]
Barua/Nyaraka kwa vikundi vidogo
Maandishi mengi yaliyofojiwa yanatoka katika maandiko ya jumla na ya umma, kama hii makala ya gazeti, (hakuna shaka habari za kughushi zisizokuwa na idadi tayari zinasambazwa kwenye soko lisilo rasmi. Mtaalamu wa Historia Louis Gottschalk anakiri kwamba barua binafsi kwa wasikilizaji wachache zina uwezekano mkubwa kuwa hakika.[19] ni Aina gani maandiko ya Agano Jipya yanaingia?
Kumbe, baadhi yake yalikusudiwa kusambazwa sehemu kubwa. Lakini sehemu kubwa ya Agano Jipya ina barua binafsi zilizoandikwa kwa vikundi na watu wachache. Maandiko haya, angalau, yasingefikiriwa muhimu kwa kukanusha.
Sehemu zinazotatiza
Waandishi wengi hawataki kujitatiza wenyewe hadharani. Wanahistoria kwa hiyo wameangalia maandiko yenye dhihirisho za kutatiza kuhusu waandishi zinapaswa kwa ujumla kuaminiwa. Kitu gani waandishi wa Agano Jipya walisema kuhusu wao wenyewe nafsi zao?
Kwa kustajaabisha, watunzi wa Agano Jipya wamejionyesha wenyewe mara nyingi kama wapuuzi, waoga na wasio na imani Kwa mfano, fikiria ukanaji mara tatu wa Peter wa Yesu au mabishano ya mitume juu ya nani kati yao alikuwa mkubwa – simulizi zote hizi zimerekodiwa katika Injili. Kama ambavyo heshima kwa mitume ilivyokuwa muhimu katika kanisa la kale, ujumuishaji wa mambo haya hauleti maana labda kama mitume walikuwa wakiripoti ya ukweli.[20]
Katika Hadithi ya Ustaarabu Will Durant aliandika kuhusu mitume,
“Watu hawa hawakuwa aina ambayo mtu angechagua kutumia kuibadili dunia. Injili kwa uhalisia inatofautisha wahusika wake, na kwa uaminifu inaonesha makosa yao.”[21]
Mambo yasiyohusika
Injili inatuambia kwamba karibu tupu la Yesu liligunduliwa na mwanamke, ingawaje nchini Israel ushuhuda wa wanawake ulichukuliwa kuwa karibia hauna thamani na ulikuwa haukubaliki mahakamani. Mama wa Yesu na familia wanarekodiwa wakinena imani yao kwamba alipoteza akili yake. Baadhi ya maneno ya mwisho ya Yesu msalabani yanasemekana yalikuwa “Mungu wangu, Mungu wangu, kwanini umeniacha?“ na hivyo hivyo inaendelea orodha ya matukio yaliyorekodiwa katika Agano Jipya hayaleti maana ikiwa kusudio la mwandishi lilikuwa kitu kingine mbali na uenezi sahihi wa maisha na mafundisho ya Yesu Kristo.
Kukosekana kwa mambo husika
Ni kinyume (au pengine ni sawa) kwamba machache katika masuala makubwa yaliyolikabili kanisa la karne ya kwanza, Misheni kwa Mataifa, zawadi za kiroho, ubatizo, uongozi – ulishughulikiwa moja kwa moja katika maneno yaliyorekodiwa ya Yesu. Ikiwa wafuasi wake walikuwa tu wakizidisha mambo ili kuhimiza ukuaji wa kanisa, haileweki kwanini hawakukusanya maelekezo toka kwa Yesu kwa masuala haya. Katika hali moja, mtume Paulo wazi wazi alisema kuhusu jambo fulani, “Kwa hili hatuna mafundisho toka kwa BWANA.”