Imepotea katika kutafsiri?
Hivyo, kitu gani ushahidi unaonesha? Tunaanza na maswali mawili rahisi: Lini maandiko ya Agano Jipya yaliandikwa? Na nani aliyaandika?
Umuhimu wa maswali haya unapaswa kuwa wazi. Ikiwa maelezo ya Yesu yaliandikwa baada ya mashahidi wa macho kuwa wamekufa, hakuna ambaye angethibitisha usahihi wake. Lakini ikiwa maelezo ya Agano Jipya yaliandikiwa na mitume waliokuwa hai, basi uhalisia wake ungeweza kuwekwa/kupatikana. Peter angeweza kusema ya kugushi kwa jina lake, “Hey, sikuandika hayo”. Na Mathayo, Marko, Luka au Yohana wangeweza kujibu maswali au changamoto zilizoelekezwa katika maelezo ya Yesu.
Waandishi wa Agano Jipya walidai kutoa maelezo ya mashahidi wa macho ya Yesu. Mtume Petro alisema hivi katika waraka mmoja: Tulikuwa hatufanyi hadithi za kijanja tulipowaambia kuhusu nguvu za Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake tena. “Tumeona utukufu wake mkuu kwa macho yetu wenyewe” (2 Petro 1:16 NLT).
Sehemu kubwa ya Agano Jipya ni barua 13 za mtume Paulo kwa makanisa machanga na vijana. Barua za Paulo, za tarehe kati ya miaka ya 40 na 60 (miaka 12 hadi miaka 33 baada ya Kristo), zimebeba ushahidi wa kwanza mapema kuhusu maisha ya Yesu na mafundisho. Will Durant aliandika umuhimu wa kihistoria wa barua za Paulo, “Ushahidi wa Kikristu kwa ajili ya Kristo unaanza na barua zilizotoka kwa Mtakatifu Paulo. Hakuna aliyehoji kuwapo kwa Paulo, au mikutano yake iliyorudiwa na Petro, James, na Yohana, na Paulo kwa kijicho anakubali watu hawa walikwishamjua Kristo katika mwili.”[2]