Tofauti ya Muda
Sio tu idadi ya maandiko ni muhimu, lakini pia tofauti ya muda kati ya kipindi andiko asilia liliandikwa na tarehe ya nakala. Zaidi ya muda wa miaka elfu moja ya kunakili, hakuna maelezo nini maandishi yangekuwa – Lakini zaidi ya miaka mia moja, hiyo ni hadithi tofauti.
Mkosoaji wa Kijerumani Ferdinand Christian Baur (1792 – 1860) mara alipodai Injili ya Yohana haikuandikwa hadi karibia A.D. 160; kwa hiyo, isingeliweza kuwa imeandikwa na Yohana. Hili, ikiwa ni kweli, lisingeliharibu maandiko ya Yohana tu, bali lingeliweka mashaka kwenye Agano Jipya lote pia. Lakini kisha, wakati makusanyo ya vipande vya Agano Jipya yalipogunduliwa Misri, miongoni mwake kulikuwa na kipande cha Injili ya Yohana (mahususi P52: Yohana 18:31 – 33) kuanzia miaka 25 kwa kukadiria baada ya Yohana kuandika andiko halisi.
Metzger alieleza, Kama Robinson Crusoe, alivyoona, lakini nyayo pekee mchangani, kulihitimisha kwamba binadamu mwingine, mwenye miguu miwili, alikuwapo katika kisiwa pamoja naye, hivyo P52 [lebo ya kipande) inathibitisha kuwapo na matumizi ya Injili ya Nne wakati wa nusu ya kwanza ya karne ya pili katika mji wa jimbo katika Naili, iliyoondolewa toka katika mahali pake asilia pa uumbaji (Efeso Asia).”[10]Kutafuta na baada ya kutafuta, akioolojia (Elimu-kale) imevumbua nakala za sehemu kubwa za Agano Jipya kuanzia ndani ya miaka 150 ya nakala halisi.[11]
Zaidi ya maandiko mengine ya kale yana tofauti za muda kuanzia miaka 400 hadi 1,400.. Kwa mfano, Ushairi wa Aristotle uliiandikwa karibu miaka 343 B.C., lakini nakala ya mwanzo ni tarehe A.D. 1100, pamoja na nakala tano tu zilizopo. na lakini hakuna mtu anayeenda kumtafuta Plato wa kihistoria, wakidai alikuwa ni mtu wa zimamoto na si mwanafalsafa.
Kwa kweli kuna nakala karibu kamili ya Biblia iliyoitwa, Codex Vaticanus, ambayo iliandikiwa karibia miaka 250 hadi 300 tu mara baada ya maandiko asilia ya mitume. Nakala ya zamani sana inayojulikana ya Agano Jipya katika maandishi makubwa ya kale inaitwa Codex Sinaiticus, sasa imehifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Uingereza.
Kama ilivyo Codex Vaticanus, inaanzia karne ya nne. Vaticanus na Sinaiticus, tukirudi nyuma katika Historia ya Kikristu ya zamani, ni kama maandishi mengine ya kale ya Kibiblia, kwamba yanatofautiana kidogo na yanatupa picha nzuri ya kile maandiko asilia hasa yalichokuwa yanasema.
Hata msomi mkosoaji John A.T. Robinson amekubali,
“Wingi wa maandiko, na zaidi ya yote, kipindi kifupi cha muda kati ya maandiko na nakala zilizopo za mwanzo, zinafanya hadi sasa yawe maandishi yaliyothibitishwa vizuri kati ya maandiko yote ya kale duniani.”[12]
Profesa wa sheria John Warwick Montgomery alihakikisha,
“kuwa mwenye mashaka kwa maandisho yote ya vitabu Agano Jipya ni kuruhusu masuala yote ya nyakati zote za kale kupotea, kwa kuwa hakuna maandiko ya kipindi cha kale yamethibitishwa vizuri kiuanishaji kama Agano Jipya.”[13]
Pointi ni hii: Ikiwa rekodi za Agano Jipya zilitengenezwa na kusambazwa kipindi karibu na matukio yenyewe, uelezaji wake wa habari za Yesu ni sahihi zaidi. Lakini ushahidi wa nje si tu njia ya kujibu swali la uhakika; wasomi pia wanatumia ushahidi wa ndani kujibu swali hili.