Mwanaakiolojia wa Biblia William Albright akihitimisha katika msingi wa utafiti wake kwamba vitabu vyote vya Agano Jipya viliandikwa wakati wengi wa mitume walikuwa hai. Aliandika, “Tunaweza kusema tayari kwa upole kwamba hakuna tena msingi wowote kwa kuwekea tarehe kitabu chochote baada ya karibia miaka 80 A.D., vizazi viwili kamili kabla ya tarehe kati ya miaka 130 na 150 A.D. iliyotolewa na wakosoaji zaidi wa Agano Jipya wa leo.”[4] Mahali pengine Albright anaweka maandiko ya Agano Jipya zima katika wakati unaowezekana sana kati ya yapata miaka 50 A.D. na 75 A.D.”[5]
Mkosoaji mbishi John A.T. Robinson anawekea kalenda Agano Jipya mapema zaidi kuliko hata wasomi wa kawaida zaidi. Akilipa tarehe upya Agano Jipya Robinson anadai kwamba mengi ya Agano Jipya yaliandikwa kati ya miaka 40 A.D. na 65 A.D. Hiyo inaweka maandiko yake mapema kama miaka saba baada ya Kristo kuishi.[6]Ikiwa hivyo ni kweli, makosa yoyote ya kihistoria yangeoneshwa haraka na wote mashahidi wa macho na maadui wa Ukristu.
Hivyo, hebu tuangalie mtiririko wa taarifa ambazo zinatuchukua toka maandiko halisi hadi kwenye nakala yetu ya Agano Jipya leo.