Lakini ni kweli?
Katika vitabu, magazeti na makala za TV, semina ya Yesu inapendekeza Injili ziliandikwa mwishoni mwa miaka A.D 130 hadi 150 na waandishi wasiojulikana. Ikiwa tarehe hizo za baadaye ni sahihi, kungekuwa na kitambo cha karibia miaka 100 tangu Kifo cha Yesu (wasomi wanaweka Kifo cha Yesu kati ya miaka A.D. 30 na 33. Na kwa sababu mashahidi wote wa macho wangekuwa wameshakufa, Injili ingekuwa imeandikwa na waandishi bandia wasiojulikana.
Hivyo, ushahidi gani tunao kuhusu lini maelezo ya Injili yaliandikwa kweli? Makubaliano ya wasomi wengi ni kwamba Injili ziliandikiwa na mitume wakati wa karne ya kwanza. Wananukuu sababu kadhaa ambazo tutaziangalia baadaye katika makala hii. Kwa sasa, hata hivyo, zingatia kwamba miundo mitatu ya msingi ya ushahidi inaonekana kujenga hali madhubuti kwa ajili ya hitimisho zake.
- Maandiko ya zamani toka kwa wapinzani kama Marcion na shule ya Valentino yananukuu vitabu vya Agano, mada na vifungu (Angalia “Tabasamu la Mona Lisa.”)
- Maandiko mengi ya vyanzo vya Kikristu vya zamani, kama Clement wa Roma, Ignatio na Polycarp.
- Waligundua nakala za vipande vya Injili vilivyowekewa tarehe za mapema mwaka 117. A.D.