Nani anahitaji iliyokosewa?
Maandiko halisi ya mitume yaliheshimiwa. Makanisa yaliyasoma, yakashirikiana nayo, kwa makini yaliyatunza na kyahifadhi mbali kama hazina iliyofukiwa.
Lakini, la, utaifishaji wa Kirumi, kifungu cha miaka 2,000, na sheria ya pili ya elimu ya nguvu-joto, (themodainamiki) imechukua gharama zake. Hivyo, leo kitu gani tunacho cha hayo maandiko asilia? Hamna. Maandishi asilia yote yamepotea (ingawaje kila wiki wasomi wa Biblia, bila shaka, wanaelekea katika Maonesho ya Kale wakitarajia moja litajitokeza/litaonekana).
Lakini Agano Jipya haliko peke yake katika hatari hii; hakuna andiko lingine la kulinganishia toka katika historia za kale lililopo leo pia. Wanahistoria hawasumbuliwi na kukosekana kwa maandiko asilia ikiwa wana nakala za uhakika kuangalia. Lakini kuna nakala za kale za Agano Jipya zinapatikana, na ikiwa ni hivyo, zinaaminika kwa nakala halisi asilia?
Kadri idadi ya makanisa ilivyoongezeka, mamia ya nakala zilitengenezwa kwa makini chini ya usimamizi wa viongozi wa kanisa. Kila herufi kwa makini iliandikwa kwa wino kwenye ngozi ya kuandikia au karatasi. Na hivyo, leo, wasomi wanaweza kusoma nakala zilizosalimika (na nakala kati ya nakala, na nakala miongoni nakala upatazo), kuhakiki uhalisia na kufikia kadirio la karibu la maandiko asilia.
Kwa kweli, wasomi wasomao uandishi wa kale wamevumbua sayansi ya ukosoaji maandishi kuchunguza maandiko kama ya Odyssey, wakiyalinganisha na maandiko mengine ya kale kuhakiki usahihi wake. Hivi karibuni, mwanahistoria ya kijeshi Charles Sanders aliongeza ukosoaji wa maandishi kwa kubuni kipimo cha sehemu tatu ambaco kinaangalia si tu uaminifu wa nakala bali pia sifa za waandishi. Vipimo vyake ni hivi:
- Kipimo cha Kitabu, kiuanishaji na kiuchapaji.
- Kipimo cha ushahidi wa ndani.
- Kipimo cha ushahidi wa nje.[7]
Ngoja tuangalie nini kinatokea wakati tunatumia vipimo hivi kwenye maandiko ya kale ya Agano Jipya.
Kipimo cha Kitabu, kiuanishaji na kiuchapaji
Kipimo hiki kinalinganisha andiko na historia ya zamani ya wakati huo huo. Linachunguza:
- Nakala ngapi za andiko asilia zipo?
- Tofauti ya wakati ni kubwa kiasi gani kati ya maandiko asilia na nakala za mwanzo kabisa?
- Jinsi gani kwa usahihi andiko linalinganisha na historia ya zamani?
Fikiria tungekuwa na nakala mbili tu au tatu za maandiko asilia ya Agano la Kale. Uchambuzi ungekuwa mdogo sana kiasi kwamba tusingeweza kuhakiki usahihi. Kwa upande mwingine, tungekuwa nazo mamia au maelfu, tungeweza kwa urahisi kuondoa makosa ya maandiko yaliyoenezwa vibaya.
Hivyo, jinsi vizuri Agano Jipya linalingana na maandiko mengine ya kale angalia kwa zote idadi ya nakala na tofauti ya wakati kuanzia nakala asilia? Zaidi ya maandiko 5,000 ya Agano Jipya yapo leo katika lugha asilia ya Kigiriki. Wakati wa kuhesabu tafsiri kwenda lugha zingine, idadi inakaribia 24,000 – kuanzia karneya pili hadi nne.
Linganisha hiyo na maandiko ya kale ya kihistoria ya pili yaliyohifadhiwa vizuri zaidi, ya Homer, nakala 643.[8] Na kumbuka kazi nyingi za historia za kale zina maandiko machache yaliyopo kuliko hizo, (mara nyingi chache chini ya kumi) Msomi wa Agano Jipya Bruce Metzger aliandika, “Kinyume na takwimu hizi [za maandiko ya kale], ukosoaji wa kiandishi wa Agano Jipya unashindwa kwa wingi wa habari zake”[9]