Katika kesi za jinai, wachache wamekataa msamaha. Mwaka 1915 George Burdick, mhariri jijini wa Gazeti la Baraza la New York, alikataa kudhihirisha vyanzo na sheria zinazovunjwa. Raisi Woodrow Wilson alitangaza msamaha wote kwa Burdick kwa makosa “yaliyokwishafanya na yale huenda alifanya” Kitu kilichofanya kesi ya Burdick iwe kihistoria ni kwamba alikataa msamaha. Hiyo ilileta kesi kwenye Mahakama Kuu, ambayo iliungana na Burdick ikisema kwamba msamaha wa Raisi usingelazimishwa kwa kila mtu.
Linapokuja suala la kukataa msamaha kamili wa Kristo, watu wanatoa aina-tofauti za sababu. Wengi wanasema hakuna ushahidi wa kutosha, lakini, kama Bertrand Rusell na kundi la wakosozi wengi, hawavutiwi vya kutosha kuchunguza hasa. Wengine wanakataa kuangalia mbele zaidi ya wakristo wanafiki wanaowajua, wakilaumu tabia zisizobadilika na zisizopendeza kama kisingizio. Na wengine bado wanamkataa Kristo kwa sababu wanamlaumu Mungu kwa matukio ya huzuni na kusikitisha waliyohangaikia.
Hata hivyo Zacharia, aliyejadiliana na wenye akili kwenye mamia ya maeneo ya vyuo anaamini kwamba sababu ya kweli ambayo watu wanamkataa Mungu ni ya kimaadili. Anaandika:
“Binadamu hamkatai Mungu kwa sababu ya mahitaji ya kiakili wala kwa uchache wa ushuhuda. Mwanadamu anamkataa Mungu kwa sababu ya ubishi wa kimaadili ambao unakataa kukubali kumhitaji kwake Mungu.”[19]
Tamaa kwa ajili ya uhuru wa kimaadili ulimweka C.S Lewis mbali na Mungu kwa sehemu kubwa ya miaka yake ya chuoni. Baada ya kutafuta kwake ukweli, kulimwongoza kwa Mungu, Lewis anaeleza jinsi gani kumkubali Kristo kulihusisha zaidi ya makubaliano ya werevu wa ukweli. Anaandika:
“Mwanadamu aangukaye si tu kiumbe asiye mkamilifu anayehitaji kustawi: ni muasi ambaye lazima alaze chini mikono yake. Kulaza chini mikono yako, kusalimu amri, kusema unasikitika, kutambua kwamba umekuwa kwenye njia potofu na unakuwa tayari kuanza maisha upya tena ndiyo kile wakristu wanaita kutubu.”[20]
Kutubu ni neno ambalo linamaanisha mkengeuko mkubwa katika kufikiri. Hicho ndicho kile kilichotokea kwa Nixon “msuluhishi wa zamani”. Baada ya Kashifa ya Watergate kuwekwa wazi, Colson alianza kufikiria kuhusu maisha kitofauti. Akitambua kukosa kwake mwenyewe kwa kusudio, alianza kusoma Ukristu wa Lewis, uliopewa kwake na rafiki. Akiwa amefundishwa kama mwanasheria, Colson alichukua muhuri wa njano na alianza kuandika mahojiano ya Lewis. Colson alikumbuka:
“Nilijua wakati ulikuwa umefika kwangu…. Nilipaswa kukubali bila majadiliano Yesu Kristo ni Bwana wa maisha yangu? Ni kama geti mbele yangu. Kulikuwa hakuna njia kulikwepa. Nilipaswa kuliingia kulipita au ningebaki nje. Labda au nahitaji muda zaidi nilikuwa najidanganya mwenyewe.”
Baada ya mabadilishano ya fikra ya ndani, huyu msaidizi kwa raisi wa Marekani, mwishowe alitambua kwamba Yesu Kristo alikuwa anastahili uaminifu wake wote. Anaandika:
“Na mapema asubuhi Ijumaa wakati nimekaa peke yangu nikikodolea macho bahari niipendayo, maneno ambayo sikuwa na uhakika nayo, niliweza kuelewa au kusema au yalitoka yenyewe mdomoni mwangu.’Bwana Yesu, ninakuamini. Ninakukubali wewe. Tafadhali njoo katika maisha yangu. Ninaamua maisha yangu yawe kwako.'”[21]