Yesu alisema kitu gani kuhusu Mungu?
Mungu ni wa busara
Wengi wanamfikiria Mungu zaidi kuwa kama nguvu fulani kuliko mtu tunayeweza kumwona na kumfurahia. Mungu ambaye Yesu alimzungumzia si kama nguvu isiyo ya kinafsi katika mvutano wa nyota ambayo uzuri wake unapimwa kwa volti. Wala is roho mwovu mkubwa asiye na huruma angani, akipendezwa kufanya maisha yetu ya huzuni.
Kwa kinyume, Mungu ni wa busara kama sisi, lakini hata zaidi ya hapo. Anafikiri, anasikia. Anazungumza katika lugha tuyonaweza kusikia. Yesu alituambia na alituonyesha namna Mungu alivyo kama. Kulingana na Yesu, Mungu ajua kila mmoja wetu, kwa siri na binafsi, na anaendelea kutufikiria sisi siku zote.
Mungu anatupenda
Na Yesu alituambia kwamba Mungu anatupenda. Yesu alidhihirisha upendo wa Mungu pote alipoenda, wakati alipowaponya wagonjwa na aliwafikia wanaumizwa na maskini.
Upendo wa Mungu ni tofauti kabisa na wetu na kwa huo (upendo) haujajengwa kutokana na mvuto au utendaji kazi. Ni wa sadaka kwa ujumla na si mbinafsi. Yesu alilinganisha upendo wa Mungu na upendo wa baba mkamilifu. Baba mzuri anataka mazuri zaidi kwa watoto wake, anajitoa sadaka kwa ajili yao na anawapatia mahitaji. Lakini kwa faida zao zaidi, anawaadabisha.
Yesu anaelezea moyo wa Mungu wa upendo kwa hadithi kuhusu kijana muasi ambaye alikataa ushauri wa baba yake kuhusu maisha na kile kilicho muhimu. Akiwa mwenye kiburi na nia binafsi, kijana alitaka kuacha kazi na “kuishi maisha ya anasa na starehe”. Kuliko kusubiri hadi baba atakapokuwa amekuwa tayari kumpa urithi wake, alianza kusisitiza kwamba baba yake ampe mapema.
Katika hadithi ya Yesu, baba alimpatia kijana wake ombi lake. Lakini mambo yalienda vibaya kwa kijana. Baada ya kuponda fedha zake kwa starehe binafsi, kijana muasi ilimbidi kuenda kufanya kazi katika shamba la nguruwe. Muda si mrefu alikuwa na njaa hata chakula cha nguruwe kilionekana kizuri kwake. Akiwa amekata tamaa na matumaini asiye na uhakika baba yake angemkubali arudi, alipakia begi lake na akaelekea nyumbani.
Yesu anatuambia kwamba sio tu baba yake alimkaribisha nyumbani, lakini kwa kweli alimkimbilia na kukutana naye kumpokea. Na kisha baba yake alipatwa na upendo mkuu na akafanya sherehe kusherehekea kurudi kwa mtoto wake.
Inafurahisha kwamba ingawaje baba alimpenda kijana wake sana, hakumfuatafuata. Alimruhusu kijana aliyempenda ausikie uchungu na atesekee matokeo ya uchaguzi wake wa uasi. Katika namna ya kufanana, maandiko yanafundisha upendo wa Mungu hautaacha/hautalegeza kamba kwa kile kilicho bora kwetu. Yataturuhusu kusotea matokeo ya chaguzi zetu zisizo sahihi.
Yesu pia alifindisha kwamba Mungu hatalegeza kamba kwa tabia yake. Tabia ni vile sisi tulivyo kwa ndani zaidi. Ni asili yetu ambapo mawazo yetu yote na matendo yetu yanaanzia. Kwa hiyo Mungu yupo kama nani -kwa ndani zaidi?
Mungu ni Mtakatifu
Kote katika maandiko (karibu mara 600), Mungu anazungumziwa kama “mtakatifu”. Mtakatifu inamaanisha kwamba tabia ya Mungu ni safi kiroho na kamilifu kwa kila njia. Isiyo na kasoro. Hii inamaanisha kwamba haendekezi fikra ambayo ni chafu au ambayo haiendani na ubora wake kiroho.
Zaidi ya hapo, utakatifu wa Mungu unamaanisha kwamba hawezi kuwa malipo na uovu. Kwa sababu ubaya ni kinyume na asili yake, anauchukia. Ni kama uchafu kwake.
Lakini ikiwa Mungu ni mtakatifu na anachukia uovu, kwanini hakufanya tabia zetu ziwe kama zake? Kwanini kuna wanajisi-watoto, wauaji, wabakaji na wapotofu? Na kwanini tunapambana hivyo kwa chaguzi za mioyo yetu? Hiyo inatupeleka kwenye sehemu nyingine ya kutafuta kwetu maana. Nini Yesu alisema kuhusu sisi?