Yesu alisema kitu gani kuhusu mwenyewe?
Ufumbuzi kamili wa Mungu
Wakati wa miaka yake mitatu ya idara ya hadhara. Yesu alitufundisha jinsi gani kuishi na kufanya miujiza mingi, hata kufufua wafu. Lakini alisema kwamba mpango wake wa msingi ni kutuokoa kutoka katika dhambi zetu.
Yesu alitangaza rasmi kwamba alikuwa Masiha ambaye angechukua uovu wetu juu yake. Nabii Isaya aliandika kuhusu Masiha miaka 700 mapema kabla, akitupa sisi siri chache kuhusu wasifu wake. Lakini siri ngumu zaidi ni kwamba Masiha angekuwa wote mtu na Mungu!
“Kwetu sisi, mtoto amezaliwa, kwetu sisi mtoto ametolewa. Na jina lake ataitwa Mwenyezi Mungu, Baba wa milele, Mtoto-Mfalme wa Amani” (Isaya 9:6).
Mtunzi Ray Stedman anaandika Masiha aliyeahidiwa wa Mungu: Tangu mwanzo kabisa wa Agano la Kale, kuna ishara ya matumaini na matarajio, kama sauti ya nyayo zikaribiazo: Mtu fulani anakuja… matumaini hayo yanaongezeka katika rekodi yote ya kinabii kama nabii baada ya nabii atangazapo kidokezo kingine kinachotamanisha: fulani anakuja!”[8]
Manabii wa kale walikwishatabiri kwamba Masiha angekuwa sadaka ya dhambi kamilifu ya Mungu, akitimiliza haki yake. Huyu mtu mkamilifu angefaulu kufa kwa ajili yetu. (Isaya 53:6).
Kulingana na waandishi wa Agano Jipya, sababu ya pekee Yesu alifaulu kufa kwa ajili ya sisi wengine ni kwa sababu kama Mungu, aliishi maisha kamilifu ya kimaadili na hakuwa mlengwa kwa hukumu ya dhambi.
Ni vigumu kuelewa jinsi gani kifo cha Yesu kililipia dhambi zetu. Labda mijadala ya kisheria ingeweza kubainisha namna gani Yesu anatatua mkanganyiko kuhusu upendo kamili wa Mungu na haki.
Fikiria unaingia chumba cha mahakama, una hatia ya mauaji (una baadhi ya masuala nyeti). Unapokaribia benchi, unatambua kwamba jaji ni baba yako. Huku ukijua kwamba anakupenda, unaanza kujitetea kwa haraka, “Baba, niache niende”.
Kwayo anajibu, “Nakupenda, kijana, lakini mimi ni jaji. Siwezi kukuacha uende kirahisi.”
Anagawanyika/anakuwa na uamuzi mgumu. Mwisho anagonga kifimbo chake na anakutangaza wewe ni mwenye hatia. Haki haiwezi kulegezwa, kwa vovyote vile hata na jaji. Lakini kwa sababu anakupenda, anatelemka kutoka katika kiti, anaondoa kamba, na anajitoa kulipa adhabu kwa ajili yako. Na kwa kweli, anakaa sehemu ile badala yako katika kiti cha umeme.
Hii ni picha iliyochorwa na Agano Jipya. Mungu alishuka katika historia ya mwanadamu, katika nafsi ya Yesu Kristo, na akaenda katika kiti cha umeme (soma: msalaba) badala yetu sisi kwa ajili yetu. Yesu si kijakazi wa upande baki, anayechukua dhambi zetu, bali ni Mungu yeye mwenyewe. Tunaweza kusema, Mungu na chaguzi mbili: kuhukumu dhambi ndani yetu au kuchukua adhabu mwenyewe. Kwa Kristo, alichagua chaguo la mbili.
Ingawaje U2’s Bono hajifanyi kuwa mwanateolojia, kwa usahihi anaeleza sababu ya Kifo cha Yesu:
“Hoja ya kifo cha Kristo ni kwamba Kristo alichukua dhambi za duni, ili kile tulichokiondoa kisirudi tena kwetu, na kwamba asili yetu ya dhambi isivune kifo dhahiri. Hiyo ni pointi. Inafaa itufanye tuwe wanyenyekevu. Si tu kazi nzuri zetu wenyewe ambazo zinatupeleka katika mageti ya Mbinguni.”[9]
Na Yesu aliiweka wazi kwamba ni yeye pekee anayeweza kutupeleka sisi kwa Mungu, akisema “Mimi ni njia, ukweli na uzima”. “Hakuna anayekuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.” (Yohana 14:6)
Lakini wengi wamebisha kwamba dai la Yesu kwamba yeye ni njia ya pekee kwa Mungu ni jembamba, wanasema kuna njia nyingi kwenda kwa Mungu. Hao wanaoamini dini zote ni sawa wanakana tuna tatizo la dhambi. Wanakataa kuchukua maneno ya Kristo kihakika. Wanasema upendo wa Mungu utatukubali sisi sote bila kujali tulichofanya.