Madonna alijaribu kujibu swali la “Kwanini nipo hapa?’ kwa kuwa mwimbaji mwanamke maarufu, akikiri, “Kumekuwa na miaka mingi wakati ambapo nilifikiri umaarufu, bahati, heri na kukubaliwa na halaiki kungeniletea furaha. Lakini siku moja unaamka na kutambua hazileti [furaha]…. Nilihisi kitu fulani kilikuwa kinakosekana…. Nilitaka kujua maana ya furaha ya kweli idumuyo na jinsi gani ningeweza kwenda kuipata.”[1]
Wengine wamekata tamaa katika kutafuta maana. Kurt Cobain, mwimbaji mwongozaji wa bendi ya Seattle ya Nirvana, alikata tamaa ya maisha katika umri wa miaka 27 na akafanikisha kujiua. Mtaalamu wa vikatuni wa enzi ya muziki wa Jazz Ralph Barton pia aliona maisha kuwa hayana maana, akaacha kimeseji cha kujiua: “Nimepata shida chache, marafiki wengi, mafanikio makubwa; nimepitia toka mwanamke mmoja hadi mwingine, nyumba hadi nyumba, nimetembelea nchi za dunia, lakini nimechoshwa na kazi ya kuendelea kubuni vifaa muda wote wa saa 24 za siku nzima.”[2]
Pascal, mwanafalsafa mkubwa wa kifaransa aliamini huu uwazi ambao wote tunakabiliana nao unaweza tu kukamilishwa na Mungu. Anaeleza, “Kuna uwazi wa Mungu katika moyo wa kila mtu ambao Yesu Kristo peke yake anaweza kuujaza.”[3] Ikiwa Pascal yuko sawa, basi tungemratajia Yesu si tu kujibu swali la utambulisho wetu na maana katika maisha haya, lakini pia anatupa tumaini kwa maisha baada ya sisi kufa.
Kunaweza kuwa na maana, bila Mungu? Si kulingana na asiyeamini Mungu Bertrand Russell, aliyeandika, “labda uchukulie kuna mungu, suala la madhumuni ya maisha halina maana.”[4] Russell alijuzulu mwenyewe mwishowe kwa ku”oza” kaburini. Katika kitabu chake, Kwanini mimi si mkristu, Russell alitupilia mbali kila kitu Yesu alisema kuhusu maana ya maisha, ikiwamo ahadi yake ya uzima wa milele.
Lakini ikiwa Yesu kwa kweli alishinda kifo kama mashahidi wa macho walivyodai, (Saa Yesu Alifufka Wafu) basi ni yeye mwenyewe angeweza kutuambia nini maisha yapo kwa sababu, na kujibu “Wapi ninaenda?” ili kuelewa jinsi gani maneno ya Yesu, maisha na kifo yanaweza kuimarisha utambulisho wetu kutupa maana katika maisha, na kutoa matumaini kwa siku zijazo, tunahitaji kuelewa kitu gani alisema kuhusu Mungu, kuhusu sisi na kuhusu yeye mwenyewe.