Labda Hitler anastahili adhabu, wanatoa sababu, lakini sio wao au wengine wanaoishi “maisha ya heshima”. Ni kama kusema kwamba Mungu anaweka gredi kwa mstari, na kila mtu anayepata D au zaidi ataingia ndani. Lakini hili linaleta mkanganyiko.
Kama tulivyoona, dhambi ni kinyume kabisa cha tabia takatifu ya Mungu. Hivyo tumemkosea yule aliyetuumba, na aliyetupenda kiasi cha kutosha kumtoa sadaka mwanawe kwa ajili yetu. Katika maana ya uasi wetu ni kama kutema kwenye uso wake. Wala si matendo mazuri, dini, kufikiria, au Karma kunaweza lipa deni dhambi zetu zilizoingia.
Kulingana na mwanateolojia R.C Sproul, Yesu pekee ndiye anayeweza lipa deni hilo. Anaandika:
“Musa aliweza kupatanisha katika sheria; Muhammad aliweza kutumia upanga; Buddha aliweza kutoa ushauri binafsi; Confucius aliweza kutoa misemo ya busara; lakini hakuna mmoja kati ya hawa watu alifaulu kutoa malipo kwa dhambi za dunia…. Kristo pekee ni mwenye thamani kwa kujitoa kusiko na kikomo na huduma.”[10]
Zawadi isiyo stahiki
Neno la kibiblia kuelezea msamaha wa bure wa Mungu kupitia kifo cha kujitoa sadaka cha Yesu ni rehema. Wakati huruma inatuokoa kutoka katika kile tunachostahili, rehema ya Mungu inatupa sisi kile ambacho hatustahili. Hebu turejee kwa dakika jinsi gani Kristo alivyotendea kile tusingeweza kufanya kwa ajili yetu:
- Mungu alitupenda na alituumba kwa ajili ya uhusiano na Yeye.[11]
- Tumepewa uhuru kukubali au kukataa uhusiano huo.[12]
- Dhambi zetu na uasi dhidi ya Mungu na sheria zake umetengeneza ukuta wa utendano kati yetu na Yeye Mungu.[13]
- Ingawa tunastahili hukumu ya milele, Mungu amelipa deni letu kwa ukamilifu kwa Kifo cha Yesu kwetu, kufanya uzima wa milele pamoja na Yeye uwezeke.[14]
Bono anatupa mtazamo wake kwenye rehema.
“Rehema inabatilisha sababu na maana Upendo inaingilia kati, ukipenda, matokeo ya matendo yako, ambao kwa mazingira yangu ni habari nzuri sana kwa sababu nimefanya mambo mengi ya kipambavu…. Ningekuwa katika matatizo makubwa iwapo Karma angekuja kunihukumu mwishowe…. Haisahaulishi makosa yangu, lakini ninaepushwa kwa rehema. Ninaepushwa/nisamehewa kwamba Yesu alichukua dhambi zangu kwenye msalaba, kwa sababu ninajua mimi ni nani, na ninatumai sihitaji kutegemea dini yangu mwenyewe.”[15]
Sasa tuna picha ya mpango wa Mungu wa muda mrefu ikijiweka pamoja. Lakini kuna kitu kimoja kinakosekana. Kulingana na Yesu na waandishi wa Agano Jipya, kila mmoja wetu pekee lazima aitikie na apokee zawadi ya bure Yesu anayotupatia sisi. Hatatulazimisha kuipokea.