Colson aligundua kwamba maswali yake, “Mimi ni nani?” “Kwani nipo hapa?” na “Wapi ninaenda?” yote yanajibiwa katika uhusiano pekee na Yesu Kristo. Mtume Paul anaandika, “Ni katika Kristo ambamo tunajua sisi ni nani na kitu gani tunaishi kwacho.” (Waefeso 1:11, Ujumbe).
Tunapoingia katika uhusiano binafsi na Yesu Kristo, anajaza pengo letu la ndani, anatupa amani, na anaridhisha hamu zetu za maana na matumaini. Na hatuhitaji kujiweka katika vichocheo vya muda kwa ajili ya kutimiliza kwetu. Anapoingia kwetu sisi, pia anatimiza matamanio yetu ya ndani na mahitaji kwa ajili ya usalama wa kweli na upendo unaodumu.
Na kitu cha kushangaza ni kwamba Mungu mwenyewe alikuja kama mwanadamu kulipa deni letu lote. Kwa hiyo, hatuko tena katika adhabu ya dhambi. Paulo anasema hili waziwazi kwa warumi pale anapoandika,
“Mlikuwa maadui wake mliotengwa kutoka kwake kwa mawazo na matendo yenu maovu, lakini sasa amewarejesha kama rafiki zake. Amefanya hili kupitia kifo chake msalabani katika mwili wake mwenyewe wa kibinadamu. Matokeo yake, amewaleta katika uwapo wa Mungu, ninyi ni watakatifu na bila lawama mkisimama mbele yake bila kosa hata moja””(Wakolosai 1:21b-22a NLT).
Hivyo Mungu alifanya kile hatukuweza kufanya kwa nafsi zetu. Tumewekwa huru kutoka katika dhambi zetu kwa kifo kitakatifu cha Yesu. Ni kama muuaji wa halaiki anayepelekwa mbele ya jaji na anapewa msamaha wote. Hastahili msamaha, wala sisi pia hatustahili msamaha. Zawadi ya Mungu ya uzima wa milele ipo bure kabisa – na ipo tayari kwa ajili ya kuchukua. Lakini ingawaje msamaha unatolewa kwetu, ni juu yetu kuukubali. Chaguo ni lako.
Upo katika mahali katika maisha yako ambapo ungependa kuikubali ofa ya bure ya Mungu?
Labda kama Madonna, Bono, Lewis na Colson, maisha yako yamekuwa bure kabisa. Hakuna kitu ulichojaribu kimeridhisha kiu ya ndani unayosikia. Mungu anaweza kuridhisha kiu hiyo na kukubadili katika muda mfupi. Alikuumba uwe na uhai ambao umejazwa na maana na makusudio. Yesu alisema, Dhumuni langu ni kutoa uzima katika ukamilifu wake wote.” (Yohana 10:10b)
Au labda mambo yanaenda vizuri kwako katika maisha lakini haujatulia na umekosa amani. Unatambua kwamba umevunja sheria za Mungu na umetengwa kutoka katika upendo na msamaha wake. Unahofia hukumu ya Mungu Yesu alisema, “Ninawaachia zawadi — amani ya akilini na moyoni. Na amani ninayotoa si kama amani dunia itoayo.”
Hivyo iwe kwamba umechoshwa na maisha ya ufuatiliaji bure au unasumbuliwa na kukosa amani kwa Muumbaji wako, jibu lipo katika Yesu Kristo.
Unapoweka imani yako katika Yesu Kristo, Mungu atakusamehe dhambi zako zote, za zamani, sasa na wakati ujao na kukufanya wewe mtoto wake. Na ukiwa kama mtoto wake akupendaye, anakupa wewe dhumuni na maana katika maisha duniani na anaahidi uzima wa milele pamoja naye.
Maneno ya Mungu yanasema, “kwa wote waliomwamini na kumkubali, aliwapa haki ya kuwa watoto wa Mungu.” (Yohana 1:12)
Msahama wa dhambi, makusudio katika maisha, na uzima wa milele yote ni yako kuuliza. Unaweza kumualika Kristo katika maisha yako sasa hivi kwa imani kupitia maombi. Maombi/Sala ni kuongea na Mungu. Mungu anajua moyo wako hahusiki kama maneno yako kwa sababu yupo pamoja na msimamo wa moyo wako. Ifuatayo ni sala iliyopendekezwa:
“Mpendwa Mungu, ninataka kukujua wewe binafsi na kuishi milele pamoja na wewe. Nakushukuru wewe, Bwana Yesu kwa kufa msalabani kwa dhambi zangu.. Nafungua mlango wa maisha yangu na kukupokea wewe kama mkombozi na Bwana. Ongoza maisha yangu na nibadili mimi, nifanye mimi aina ya mtu unayetaka niwe.”
Maombi haya yanaeleza hitaji la moyo wako? Ikiwa ni hivyo, sali maombi yaliyopendekezwa hapo juu kwa lugha yako ya asili.
Mara Chuck Colson alipotoa maisha yake kwa Kristo, mtu huyu ambaye alishamtumikia Raisi wa Marekani, sasa alifurahi katika kumtumikia Mungu wa ulimwengu. Alianza kuwasaidia wengine kugundua uhuru na furaha aliyogundua katika Kristo.
Baada ya kutumikia muda gerezani kwa makosa yake ya kashifa ya Watergate, Mungu alimpa Colson upendo mpya na kujali kwa ajili ya wafungwa. Kujali kwake kupya kwa hao waliokwamisha jamii kulimfanya kuanzisha Ushirika wa Magereza,” idara ambayo imeshirikiana kujua ukweli na rehema za Yesu Kristo kwa mamilioni ya wafungwa duniani kote.
Yesu pia amefanya imewezekana kwako kupata maisha ya maana, madhumuni na nguvu. Anakupenda wewe na ana mpango wa kupendeza kwa ajili ya maisha yako ambao unaweza kuanza upya leo, bila kujali kushindwa kwako kwa zamani na dhambi.
Kiunganishi hapa chini kinatoka taarifa bure ambazo zitakusaidia wewe kugundua ahadi za msingi za kibiblia kuhusiana na safari yako pamoja na Kristo.
Je ni kweli Yesu alifufuka toka katika Wafu?
Mashahidi wa macho kwa Yesu Kristo kwa kweli walizungumza na walitenda kama walivyoamini, walimwabudu kama “Bwana” lakini lazima tuuchukue ufufuko wa Yesu Kristo kwa imani pekee, au kuna ushahidi mzito wa kihistoria?. Wakosoaji wachache walianza uchunguzi kwenye rekodi za kihistoria kuthibitisha maelezo ya ufufuko ni uongo. Ni kitu gani waligundua?
Bonyeza hapa kuchunguza ushahidi kwa madai makubwa yaliyowahi kufanywa — ufufuko wa Yesu Kristo!
Kulikuwa na Hila za Da Vinci ?
Kulikuwa na Hila za Da Vinci ambazo zilibadilisha historia ya kweli ya ukristu? Je Constantine aliagiza uharibifu wa rekodi za kweli za Yesu Kristo akatuachia historia ya uongo ya Yesu Kristo na mitume?
“Kulikuwa na hila za Da Vinci,” inachunguza dhana za hila za dunia zinaoongoza kuhusu Yesu Kristo, ikijibu madai yake kwa ushahidi.
Bonyeza hapa kugundua ukweli kuhusu Hila za Da Vinci?.
Unapoamua kujitoa kwa Yesu Kristo, anaingia katika maisha yako, anakuwa mwongozo wako, mshauri wako, mfariji wako, na rafiki yako bora zaidi. Zaidi ya hapo, anakupa wewe nguvu kushinda majaribu, vishawishi, anakuweka huru kukabili maisha mapya yaliyojaa maana, madhumuni na nguvu.
Chuck Colson aligundua madhumuni mapya na nguvu. Colson anakiri kwamba kabla ya kuwa mkristu, alikuwa mwenye tamaa, majivuno na mbinafsi. Alikuwa hana haja wala hamu ya kuwapenda wengine wanaohitaji. Lakini mawazo yake na motisha zake kwa kiasi kikubwa zilibadilika mara alipojitoa kwa Kristo.
« Previous | Next »