Uasi dhidi ya Sheria za Maadili za Mungu
C.S. Lewis alitoa sababu kwamba ingawaje ndani tumeumbwa na hamu kumjua Mungu, tunaasi dhidi yake tangu kipindi tunazaliwa.[7] Lewis pia alianza kuchunguza vichocheo vyake mwenyewe ambavyo vilimwongoza kwenye ugunduzi kwamba kwa hulka-asilia alijua mema mbali na mabaya.
Lewis alijiuliza wapi fahamu hii ya mema na mabaya ilitoka. Wote tunaisikia fahamu hii ya mema na mabaya wakati tunaposoma Hitler akiuua wayahudi milioni sita, au shujaa akijitoa akitoa sadaka maisha yake kwa ajili ya mtu fulani. Kwa hulka-asili tunajua ni vibaya kusema uongo na kudanganya. Kutambua huku kwamba tumetengenezwa pamoja na sheria ya ndani ya maadili kulimfanya mwamini miungu wa mwanzo afikie hitimisho kwamba lazima kuna “mtoa sheria ya maadili.”
Hasa, kulingana na wote Yesu na Maandiko, Mungu ametupa sheria ya maadili kuitii. Na si tu tumegeuza migongo yetu kwa uhusiano pamoja naye, pia tumevunja sheria hizi za maadili kwamba Mungu ameziweka. Wengi wetu twajua baadhi ya Amri Kumi za Mungu:
“Usiseme uongo, usiimbe, usiue, usizini,” etc. Yesu aliweka kwa ufupi kwa kusema tumpende Mungu kwa moyo wetu wote na jirani zetu kama sisi wenyewe tunavyojipenda. Dhambi, kwa hiyo si tu mbaya tuifanyao katika kuvunja sheria, lakini pia kushindwa kwetu kufanya mema yaliyo sahihi.
Mungu aliumba ulimwengu pamoja na sheria ambazo zinaongoza kila kitu ndani yake. Hazivunjwi na wala hazibadilishiki. Wakati Einstein alipokokotoa fomyula E=MC2, alivumbua siri ya nguvu za nyukilia. Kuweka michanganyiko sahihi pamoja katika mazingira yahitajiyo nguvu na nguvu kubwa inapatikana. Maandiko yanatuambia kwamba sheria ya maadili ya Mungu ni muhimu kwa sababu inatokana na tabia yake.
Tangu mwanamme na mwanamke wa mwanzo, hatukutii sheria la Mungu, ingawaje ni nzuri kwa ajili yetu. Na tumeshindwa kufanya yaliyo sahihi. Tumerithi hali hii tangu mtu wa kwanza, Adam. Biblia inaita kutotii huku, dhambi, ambayo inamaanisha “kukosa shabaha” kama mwindaji anavyokosa shabaha yake aliyokusudia. Hivyo, dhambi zetu zimevunja uhusiano wa Mungu aliokusudia pamoja na sisi. Tukitumia mfano wa mwindaji, tumekosa shabaha linapokuja suala la madhumuni tuliyoumbiwa kwayo.
Dhambi inasababisha kusitisha mahusiano yote: maisha ya mwanadamu yalikoma katika mazingira yake (kutengwa), kila mmoja alijitenga mbali wengine (kukosa na aibu), watu walijitenga na watu wengine (vita, mauaji), na watu walijitenga na Mungu (kifo cha kiroho). Kama viungio katika mnyonyoro, mara kiungio cha kwanza kati ya Mungu na ubinadamu vilipovunjika, mkusanyiko wa viungio vyote vikawa vimejitenga.
Na tumekatishwa. Kama Kanye West anavyorapu, “Na sifikiri kuna kitu chochote ninachoweza kufanya kuyapendezesha makosa yangu. Ninataka kuzungumza kwa Mungu lakini ninaogopa hatujaongea naye muda mrefu….” Mashairi ya nchi za magharibi yanazungumzia utengano ambao dhambi inaleta katika maisha yao. Na kulingana na Biblia, utengano huu ni zaidi ya ushairi katika wimbo wa kurapu/kufoka. Una matokeo ya hatari zaidi.
Dhambi zetu zimetutenga na upendo wa Mungu
Uasi wetu (dhambi) umetengeneza ukuta wa utendano kati ya Mungu na sisi (Angalia Isaya 59:2). Katika Maandiko, “Kutengwa” kunamaanisha kifo cha kiroho.. Na kifo cha kiroho kinamaanisha kutengwa kabisa kutoka katika nuru na maisha ya Mungu.
“Lakini subiri dakika moja,” unaweza kusema “Mungu hakujua yote ya hayo kabla hajatuumba?
Kwanini hakuona mpango wake ulilaumiwa kwa kushindwa?” Bila shaka Mungu ajuaye yote angetambua kwamba tungeasi na kutenda dhambi. Kwa kweli, ni kushindwa kwetu ambako kunafanya mpango wake uchanganye sana akili. Hii inatufanya tufikie sababu kwamba Mungu alikuja dunia katika umbile la mwanadamu Na hata kwa kushangaza-—sababu yake kuu isiyo ya kawaida ya kifo chake.