Unachagua hatima
Tunaendelea kufanya chaguo—kitu gani cha kuvaa, kitu gani cha kula, fani zetu, mwenzi wa ndoa, n.k. Ni sawa sawa wakati inapohusu uhusiano na Mungu. Mwandishi Ravi Zacharias anaandika:
“Ujumbe wa Yesu unadhihirisha kwamba kila mmoja… anakuja kumjua Mungu si kwa sababu ya kuzaliwa kwake, lakini kwa chaguo hai ili kumruhusu Yeye Mungu awe na taratibu katika maisha yake.”[16]
Chaguo zetu mara nyingi zinaathiriwa na wengine. Lakini katika mazingira fulani tunapatiwa ushauri mbaya. Tarehe 11 Septemba, 2001, watu wasio na hatia 600, waliweka imani yao katika ushauri potofu, na bila hatia walihangaikia matokeo yake. Hadithi ya kweli inaendelea kama hivi:
Mtu mmoja ambaye alikuwa katika sakafu/ghorofa ya 92 ya jengo ka kusini la Kituo cha Biashara Duniani (WTC) alikwishasikia mpasuko katika jengo la kaskazini. Akishangazwa na mlipuko, aliwaita Police kwa ajili ya maelekezo kuhusu ni afanye. “Tunahitaji kujua ikiwa tunahitaji kutoka hapa, kwa sababu tunajua kuna mlipuko,” alisema kwa kwa haraka mara moja kwenye simu.
Sauti katika upande mwingine ulimshauri asitoke. “Nitasubiri hadi nipate taarifa zaidi.”
“Yote sawa” msemaji alisema. “Usitoke.” Kisha akakata/akatundika simu.
Muda mfupi baada ya saa 3:00 asubuhi, ndege nyingine ikajikita katika sakafu ya 80 ya jengo la kusini. Karibia watu wote 600 katika sakafu za juu za jengo-mnara la kusini waliangamia. Kushindwa kutoka katika jengo kulikuwa ni mojawapo ya misiba mikubwa ya siku hiyo.[17]
Watu hao 600 waliangamia kwa sababu walitegemea taarifa zisizo sahihi ingawaje zilitolewa na mtu ambaye alikuwa akijaribu kusaidia. Msiba usingetokea ikiwa waathirika 600 wangekuwa wamepewa taarifa sahihi.
Chaguo letu hai kuhusu Yesu ni muhimu zaidi kuliko lile moja lililowakabili waathirika waliotaarifiwa vibaya wa Septemba 11. Kuishi milele kuko mashakani. Tunaweza kuchagua moja kati ya miitikio mitatu. Tunaweza kumdharau. Tunaweza kumkataa. Au, tunaweza kumkubali.
Sababu kubwa watu wengi wanapitia katika maisha wakimdharau Mungu ni kwamba wako kazini sana wakilazimisha agenda zao. Chuck Colson alikuwa kama hao. Katika umri wa miaka 39, Colson alichukua ofisi karibu na Raisi wa Marekani. Alikuwa ni “kijana shupavu” wa ikulu ya Nixon, “mtu wa maamuzi magumu” ambaye angeweza kufanya maamuzi magumu. Lakini kashifa ya Watergate iliharibu sifa yake na maisha yake yakawa hayana mwelekeo. Baadaye akaandika:
“Nimekuwa nikijijali nafsi yangu. Nimefanya hili na hilo, nimefaulu, nimefanikiwa na sijampa Mungu heshima yoyote, hata mara moja sijamshukuru kwa zawadi zake kwangu. Sijafikiria kitu chochote kuwa kikubwa sana kwangu, au hata kama katika nyakati fupi nilifikiria kuhusu mamlaka makubwa ya Mungu, sijamhusianisha Yeye na maisha yangu.”[18]
Wengi wanaweza kutambua hilo pamoja na Colson. Ni rahisi kukamatwa katika hatua za haraka za maisha na kuwa na muda kidogo au hakuna muda kwa ajili ya Mungu. Lakini bado kudharau zawadi ya rehema za Mungu ya msamaha una matokeo makubwa sawa na kukataa moja kwa moja. Deni letu la dhambi lingebaki bado bila kulipwa.