Uthibitisho katika gudulia
Tumeangalia katika ushahidi kwa ajili ya utimizaji wa Yesu wa tabiri za kimasiha kutoka katika kila pembe isipokuwa mmoja. Kuna nini ikiwa mwandishi wa historia mKristu ambaye alinakili maandiko ya Isaya na vitabu vingine vya Agano la kale alivibadilisha kuvifanya vifanane na maisha ya Yesu?
Hili ni swali wasomi wengi na wakosoaji wameuliza. Na inaonekana inawezekana, hata inakubalika kwa kuitazama mwanzoni. Ingetuzuia sisi kumfanya Yesu ni tapeli mdanganyifu, ambayo inaonekana haiwezi kuwa hivyo kwa kiasi kikubwa. Hivyo, jinsi gani tunajua kwamba vitabu vya kinabii vya Agano la Kale, kama vile Isaya, Daniel, na Mika viliandikwa mamia ya miaka kabla ya Kristo, kama ilivyoonekana? Na ikiwa viliandikwa, jinsi gani twajua waKristu hawakubadili maandishi baadaye?
Kwa miaka 1,900, wakosoaji wengi walishikilia sana wazo hilo, ikizingatiwa katika kusikowezekana kwa binadamu kutabiri kwa usahihi matukio ya siku zijazo. Lakini kisha kitu fulani kikatokea ambacho kilizima udadisi wote wa njama za siri. Kitu kilichoitwa Maandiko ya Bahari iliyokufa.
Nusu karne kurudi nyuma, kuonekana kwa Maandishi ya Bahari iliyokufa kuliwapatia wasomi wa Biblia nakala za vitabu vya Agano la kale ambavyo vilikuwa vya zamani kuliko vingine vinavyojulikana kuwapo. Majaribio makubwa yalithibitisha kwamba nyingi ya nakala hizi zilitengenezwa hata kabla ya Yesu Kristu hajaisha. Na kwa kweli yanafanana na maandishi ya Biblia tuliyokuwa tayari tunatumia.
Matokeo yake, hata wasomi ambao wanamkana Yesu kuwa Masiha wanakubali maandishi haya ya Agano la Kale kuwa yametangulia kuzaliwa kwake na hivyo kukubali kwamba tabiri kuhusu Masiha ziliwekwa ndani yake hazijabadilishwa ili kuendana na Yesu.
Ikiwa tabiri hizi zilitimizwa kwa usahihi kupitia maisha ya Yesu, inaonekana ni sahihi kustaajabu kwanini kila mmoja nchini Israeli hakuweza kuona hili. Lakini kama kusulubishwa kwake kunavyotoa ushahidi, si kila mmoja alikuona [kusulubishwa huko]. Kama mtume Yohana alivyosema kuhusu Yesu, “Hata katika ardhi yake mwenyewe na miongoni mwa watu wake, hakukubaliwa.” (Yohana 1:11, NLT). Kwanini?