Mitume kulinganisha na Watabiri?
Kupima kwamba usahihi wa watabiri wa kisasa unakaribia ule wa mitume wa Biblia, tumchukue Jean Dixon kama mfano halisi wa kujifunzia. Mtabiri huyu wa Kimarekani anaonekana kuwa na uwezo maalumu wa kutabiri mambo. Lakini kwenye uchambuzi sifa yake inaonekana haijathibitika.
Kwa mfano, Dixon alikuwa na maono kwamba mwezi Februari tarehe 5, 1962, mtoto alizaliwa Mashariki ya Kati ambaye angeibadili dunia kabla ya mwaka 2000. Huyu mtu maalumu angeunda dini ya dunia moja na kuleta amani ya dunia ya kudumu. Alikuwa ni msalaba unaokuwa juu ya mtu huyu hadi ufunike dunia nzima. Kulingana na Dixon, mtoto huyu angekuwa ni uzao wa malkia wa zamani wa Misri Nefertiti.[1] Yuko wapi jamaa huyu? Umemwona? Na vipi kuhusu hiyo amani ya dunia idumuyo – ni nzuri, eeh?
Kwa kweli, utafutaji mkubwa wa tabiri zake unatoa habari mbili zisizopingwa. Kiasi chake cha usahihi ni sawa na hao wanaokisia siku zijazo, na kutangaza zaidi kwa kutimia kwake kama tabiri zinavyokusudia kukisia idadi yoyote ya matukio yanayotokea kuwa ndiyo kutimia huko. Hata tabiri zilizotangazwa sana za Nostradamus zimekuwa mara nyingi zikithibitishwa kuwa sio sahihi licha ya madai yake yasiyo na uhakika, ambayo ni vigumu kuyakana kudai ni uongo.[2] Kwa mfano, hapa kuna moja ya tabiri za Nostradamus:
“Inahitaji Mungu-mke wa mbalamwezi, kwa siku yake na kutembea kwake: mzururaji na shahidi wa sheria ya Mungu, katika kuamsha maeneo makubwa ya ulimwengu kwenda kwa nia ya Mungu.”[3]
Hii inasemekana kuwa kuhusu kifo cha Binti Mfalme Diana. (Ulikuwa unafikiri inawezekana ni Margaret Thatcher.) Tabiri kama hii haziko wazi; ni kama kuona kitu katika mawingu. Lakini baadhi wanasisitiza huu ni ushahidi wa utabiri wa Nostradamus umetimizwa. Unafikiriwa sana, lakini ni vigumu kupinga kudai ni uongo.
Na hii ndiyo rekodi hasa ya mwenendo wa watabiri. Wakati “Kitabu cha Watu” kilipofanyia utafiti wa tabiri za watabiri 25 wa juu, asilimia 92 ya tabiri zilithibitishwa kuwa sio sahihi. Asimilia 8 zingine zilihojiwa na zingeweza kuelezewa kwa bahati au elimu ya jumla ya mazingira. [4] Katika majaribio mengine ya watabiri wa dunia maarufu wa kwanza, kiasi chao cha usahihi kimeonyeshwa kupita asilimia 11, ambayo inaweza kuwa sio wastani mbaya isipokuwa kwa ukweli kwamba watu wafanyao kukisia kwa haraka haraka kuhusu siku zijazo wanafikia katika asilimia ile ile. Hii haipingi kuelezea kote kwa siku zijazo, lakini kwa uhakika inaelezea kwanini watabiri hawashindi bahati nasibu.
Tofauti kati ya watabiri na mitume inaonekana kuwa zaidi ya aina moja kuliko aina ya digrii. Mitume walifanya matangazo maalumu kuhusu matukio ya siku zijazo kuhusiana na mpango wa Mungu unaonea toka katika hali madhubuti na walifanya hivyo kwa usahihi usioyumba. Watabiri ni zaidi ya mamluki, wanaotoa maelezo yasiyo hakika ya siku zijazo kwa soko lililo tayari kulipia huduma zao. Wanatoa taarifa za udadisi, lakini na rekodi yenye makosa.