Wezekano ni zipi?
Hebu tuangalie tabiri mbili maalumu kuhusu Masiha katika Agano la Kale.
“Wewe, O Bethlehem Ephrathah, ni kijiji kidogo tu nchini Yuda. Lakini bado mtawala wa Israeli atakuja toka kwako, mmoja ambaye asili zake ni kutoka nyakati za zamani za mbali.” (Mika 5:2, NLT)
“BWANA mwenyewe atachagua ishara. Angalia! Bikira atapata mtoto! Atazaa mtoto mwanamume na atamwita Immanueli – Mungu pamoja nasi.’” (Isaya 7:14, NLT)
Sasa, kabla ya kufikiria tabiri zingine 59, usimame na ujiulize watu wangapi katika aina ya Masiha watarajiwa katika historia yote walizaliwa na bikira katika mji wa Bethlehem. “Haya, hebu tuone, kuna jirani yangu George, lakini…. hapana, ngoja; alizaliwa Brooklyn.” Katika suala la tabiri 61 zilielezewa kwa kina kutimizwa na mtu mmoja, tunazungumzia hasa kuhusu nafasi zisizowezekana.
Wakati wanasayansi stadi walipogundua mlinganisho wa muundo wa DNA, wezekano za kuwa na mtu ambaye siye mara nyingi ni chini ya moja katika bilioni kadhaa (kitu kwa wapotoshaji kuweka akilini). Ingeonekana tuko kati mazingira yale yale jirani ya wezekano na sifuri, katika kufikiria mtu mmoja kutimiza tabiri hizi.
Profesa wa hisabati Peter Stoner aliwapa wanafunzi 600 swali la hisabati la uwezekano ambalo lingeng’amua uwezekano kwa mtu mmoja kutimiza tabiri nane maalumu. (Hii sio kama kurusha sarafu mara nane katika mlolongo na kupata kichwa kila mara.) Kwanza wanafunzi walikokotoa wezekano za mtu mmoja kutimiza masharti yote ya utabiri mmoja maalum, kama vile kusalitiwa na rafiki kwa vipande 30 vya fedha. Kisha wanafunzi walifanya vizuri zaidi kukadiria wezekano kwa tabiri zote nane kwa pamoja.
Wanafunzi walikokotoa kwamba wezekano kwa mtu mmoja kutimiza tabiri nane zote ni za kinyota- moja kwa kumi kwa kipeo cha 21.(1021). Kuelezea hiyo idadi, Stoner alitoa mfano ufuatao: “Kwanza, funika ardhi ya Dunia nzima kwa dola za fedha urefu wa futi 120. Pili, kwa madhumuni maalum, wekea alama mojawapo ya dola hizo na ifukie haraka haraka bila umakini. Tatu, mwambie mtu asafiri dunia nzima na kuchagua dola iliyowekewa alama huku akiwa amefungwa macho – haoni, kutoka katika trililioni za dola zingine”[7]