Utabiri wa Kidini katika Mtazamo
Utabiri unaweza kuwa mafumbo kumshirikisha Mungu, wa kimantiki na kwa kukosa neno zuri, wa kutia hofu. Unaonesha picha za mahali na limwengu zingine. Katika Vita ya Nyota kuna utabiri wa moja itayoleta urari kwenye Nguvu. Sinema za Bwana wa Ulingo zinaweka hali zao za kufikirika katika mandhari za maneno ya kitabiri. Lakini hiyo ni dunia ya kufikirika.
Kuhusiana na dunia ya kweli, imesemekana kwamba ikiwa mtu angejua hata dakika moja ya wakati ujao angetawala dunia. Fikiria hilo. Kila dakika ya kujua kila mkono uliochangwa katika Kasino ya Kupiku. Ungekuwa mtu tajiri zaidi duniani na Donald angekuwa mtumishi wa Posta.
Lakini katika ulimwengu wa dini, utabiri unasaidia kazi muhimu. Inakuwa njia moja ya uhakika kujua ikiwa mtu anazungumza toka kwa Mungu au sio, kwa kuwa Mungu ajuaye yote angeweza kujua wakati ujao barabara. Na kwa hoja hii utabiri katika Agano la Kale unabaki kuwa wa kipekee, kwa kuwa vingi kati ya vitabu vitakatifu toka katika deni zingine hazina utabiri unaobashirika. Kwa mfano, wakati Kitabu cha Nabii Mormon na Hindu Veda vinadai maongozi matakatifu, hakuna namna kuthibitisha madai yao; unaachwa tu ukihisi “Ndio, hicho ni kama kitu ambacho Mungu angeweza kusema.
Msomi wa Biblia Wilbur Smith alilinganisha tabiri za Biblia na vitabu vingine vya kihistoria, akisema kwamba Biblia ni “mkusanyiko pekee uliotengenezwa na binadamu, au kundi la watu, ambamo ndani yake kunapatikana mkusanyiko mkubwa wa tabiri kuhusiana na taifa moja moja, Israel, watu wote wa dunia, miji fulani, na kuja kwa mmoja ambaye angekuwa Masiha.”[5] Hivyo, Biblia inaweka wazi maelezo yake kwa kuongoza katika namna ambayo inaweza aidha kuthibitishwa au kukanushwa.
Na ukiweka kiwango cha usahihi katika mtazamo wa kila siku, unaweza kuona jinsi gani inavyoshangaza. Kwa mfano, ingekuwa ajabu ikiwa mwaka 1910 ulitabiri kwamba mtu aitwaye George Bush angeshinda uchaguzi wa mwaka 2000. Lakini fikiria ungeweka baadhi ya haya maelezo katika utabiri wako:
- Mgombea mwenye karibu kura zote jumla angeshindwa uchaguzi.
- Mitandao yote ya Televisheni ingetangaza mshindi na kisha kugeuka.
- Nchi moja (Florida) ingeongoza uchaguzi.
- Mahakama Kuu ya Marekani mwishowe ikaamua mshindi.
Ikiwa hivyo ingetokea, kungekuwa na makanisa yaliyopewa majina yako na midori kwenye deshibodi ingekuwa na sura yako. Lakini haukuweka, hivyo hakuna. Kama ilivyo vigumu (au haiwezekani) kama ambavyo ingekuwa mwaka 1910 kuwa imetabiriwa kwa usahihi mlolongo sahihi wa matukio, uwezekano wa mambo kuwa hivyo ungekuwa mgumu kwa Yesu, au mtu yeyote kuwa ametimiza tabiri zote za waebrania kwa ajili ya Masiha. Zilizowekwa ndani ya Agano la Kale, zilizoandikwa mamia ya miaka kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, ni tabiri mahususi 61 na karibu kumbukumbu 300 kuhusu Masiha.[6]
Kulingana na mahitaji ya waebrania kwamba utabiri lazima uwe na asilimia 100 kiwango cha usahihi, Masiha wa kweli wa Israeli lazima atimize yote au vinginevyo si Masiha. Kwa hiyo swali kwamba aidha inamthibitisha au inamfanya astahili kulaumiwa kwa udanganyifu mkubwa duniani?