Watu wanaweza kufanya vitu vizuri na namba (hasa na jina la mwisho kama hilo), hivyo ni muhimu kufahamu kwamba kazi ya Stoner ilikaguliwa na Chama cha Kisayansi cha Marekani, ambacho kilisema, “Uchambuzi wa kihisabati…umewekwa kwenye kanuni za uwezekano ambazo zote zina maana na Profesa Stoner ametumia kanuni hizi katika njia ya ifaayo na namna inayoridhisha.”[8]
Pamoja na hiyo kama utangulizi, tuongeze tabiri sita zaidi kwa hizo mbili tulizofikiria tayari ili itupe jumla ya nane za Profesa Stoner:
Utabiri: Masiha angekuwa kutoka uzao wa Mfalme Daudi.Yeremia 23:5
600 B.C. |
Kutimia: “Yesu …mwana wa Daudi…”Luka 3:23, 31
4 B.C. |
|
Utabiri: Masiha angesalitiwa kwa vipande 30 vya fedha.Zakaria 11:13
487 B.C. |
Kutimia: “Walimpa vipande thelathini vya fedha.”Mathayo 26:15
30 A.D. |
|
Utabiri: Masiha angetobolewa mikono na miguu yake.Zaburi 22:16
1000 B.C. |
Kutimia: “Walikuja sehemu iliyoitwa Golgotha. Wote watatu walisulubishwa pale – Yesu kwenye msalaba wa katikati, na wahalifu wawili kila upande.”Luka 23:33
30 A.D. |
|
Utabiri Watu wangepiga kura kwa ajili ya vazi la Masiha.Zaburi 22:18
1000 B.C. |
Kutimia “Askari… walichukua vazi lake, lakini lilikuwa halina mshono, limefumwa katika muundo mmoja kuanzia juu. Hivyo wakasema, ‘Tusilichane bali turushe daisi kuona nani analipata.’”Yohana 19:23-24
30 A.D. |
|
Utabiri: Masiha angeonekana akiendesha punda.Zakaria 9:9
500 B.C. |
Kutimia “Walileta wanyama wao kwake na wakatandika mavazi juu ya farasi wadogo, akakaa juu yake.”Mathayo 21:7
30 A.D. |
|
Kutabiri: Mjumbe angetumwa kwenda kumsalimu Masiha.Malaki 3:1
500 B.C. |
Kutimia: Yohana akawaambia, “Ninabatiza kwa maji, lakini pale katika kundi la watu kuna mtu hamumjui.”Yohana 1:26
27 A.D. |
Tabiri nane tulizorejea kuhusu Masiha ziliandikwa na watu kutoka nyakati na mahali tofauti kati ya miaka 500 na 1,000 kabla Yesu hajazaliwa. Hivyo hakukuwa na nafasi ya kula njama miongoni mwao. Angalia pia, mpangilio maalum. Hii si aina ya utabiri wa Nostradamus – “Ambapo mwezi unakuwa kijani, harage la lima linalala likifunikwa kando ya barabara.”