Kwa kufikiria historia iliyoimarishwa ya Israeli, si vigumu kusoma katika maana ya Masiha wazo la mpigania uhuru wa kisiasa. Inaeleweka jinsi gani karne ya kwanza mtu wa kiyahudi angeweza kufikiri, jinsi gani Masiha angekuja na Israeli bado ikakandamizwa chini ya ukaliaji wa Kirumi?
Wakati Yesu alipotimiza tabiri za kimasiha, alifanya hivyo katika namna ambazo hakuna yeyote alikuwa akitarajia. Alitafuta mapinduzi ya kimaadili na kiroho, si ya kisiasa, akitimiza malengo yake kwa sadaka binafsi na huduma ya kinyenyekevu, akiponya na kufundisha. Wakati huo huo, Israeli ilikuwa ikitafuta Musa mwingine au Joshua ambaye angewaongoza katika ushindi kupata tena himaya yao iliyopotea.
Bila shaka, wengi wa wayahudi kipindi cha Yesu walimtambua yeye kama Masiha – msingi mzima wa kanisa la kikristo ukiwa wa kiyahudi. Wengi wao, hata hivyo, hawakumtambua. Na si vigumu sana kuelewa kwanini.
Kuelewa vizuri matatizo kwa wayahudi karne ya kwanza, angalia huu utabiri wa kimasiha ulioandikwa miaka 700 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu na mtume Isaya. Ilikuwa inamzungumzia Yesu?
“Sisi sote tumepotea mbali kama kondoo. Tumeacha njia za Mungu kufuata zetu wenyewe. Lakini bado Bwana aliweka kwake hatia na dhambi zetu sisi sote”
“Aliteswa na kutendewa kikatili, lakini hakusema neno. Aliongozwa kama mwanakondoo kwenda machinjioni. Na kama kondoo alivyo kimya mbele ya mkata manyoya, hakufungua mdomo wake. Tokea gerezani na katika mashitaka walimpeleka mbali kwenye kifo chake. Lakini nani miongoni mwa watu alitambua kwamba alikuwa akifa kwa ajili ya dhambi zao na kwamba alikuwa akiteseka kwa adhabu yao? Hakufanya kosa, na hakuwahi kumdanganya yeyote. Lakini alizikwa kama mhalifu; aliweka kwenye kaburi la mtu tajiri.”
“Lakini ilikuwa mpango mzuri wa Bwana kumnyong’onyesha na kumjaza huzuni. Lakini wakati maisha yake yanafanywa sadaka kwa ajili ya dhambi, atakuwa na umati wa watoto, warithi wengi. …Na kwa sababu ya kile alichokiona, mtumishi wangu mwenye haki atafanya iwezekane wengi kuhesabiwa wenye haki, kwa sababu atabeba dhambi zao zote.” (Sehemu za Isaya 53:6-11, NLT)
Wakati Yesu alipokuwa akining’inia msalabani, baadhi kama inavyoeleweka wamekuwa wakifikiri, “Jinsi gani huyu anaweza kuwa Masiha? Kwa wakati ule ule, wengine huenda wamekuwa wakishangaa, “Nani mwingine kama si Yesu Isaya angekuwa anamzunguzia?’