Kwani Ukristu ulishamiri?
Morison alichanganywa na ukweli kwamba “harakati ndogo sana ziliweza kutamba dhidi ya hatamu hodari za himaya za kiyahudi, pia mamlaka za Kirrumi. “Kwanini ilishamiri katika mazingira yote hayo yaliyokuwa kinyume chake?”
Aliandika, “Ndani ya miaka ishirini, madai ya hawa wakulima wa Galilaya yalisambaratisha kanisa la kiyahudi… ndani ya miaka hamsini ilianza kutishia amani ya Himaya ya Warumi. Wakati tunaposema kila kitu kinaweza kuzungumzwa… tunabaki kushangazwa na siri kubwa kuliko zote. Kwani ukristu ulishamiri?”[33]
Kwa namna zote, Ukristu ungefia msalabani wakati ule wafuasi walipokimbia kuokoa maisha yao. Lakini mitume waliendelea kuimarisha harakati za ukuaji wa ukristu.
J.N.D Anderson, aliandika “Fikiria upuuzi wa kisaikolojia ukielezea kikundi kidogo cha waoga walioshindwa, wakiogopa ndani ya chumba cha juu siku moja na siku chache baadaye wakabadilika kuwa kampuni ambalo hakuna kitisho chochote kingeweza kuwanyamazisha – na kisha wakijaribu kuelezea hili tukio kubwa liwe bure kwa habari ya kutunga ya kusikitisha…hilo kwa ufupi lisingeleta maana.”[34]
Wanafunzi wengi wanaamini (maneno ya watoa maoni wa kale) kwamba damu ya wahanga ilikuwa ndiyo mbegu/chanzo cha kanisa. Mwanahistoria Will Durant aliona, Kaizari na Kristo walikutana katika ukumbi na Kristo alishinda.”[35]
Hitimisho la kushangaza
Pamoja na hadithi, maluweluwe na maono binafsi yaliyotawala, na ushahidi usiopingika kuhusu kaburi kubaki tupu, pamoja kundi kubwa la mashahidi kwa kuonekana kwa Yesu mara ya pili, pamoja na mageuzi yasiyoelezeka na mchango mkubwa duniani kwa hao waliodai kumwona, Morison alipata kuamini kwamba msimamo wa kubabaisha kupinga ufufuko wa Yesu, ulikuwa unafanya makosa. Alianza kuandika kitabu tafauti kilichoitwa Nani aliondosha Jiwe? Kuelezea hitimisho zake. Morison kwa ufupi alifuata mtiririko wa ushahidi, habari kwa habari hadi ukweli wa jambo hili ukaonekana wazi kwake. Hitimisho likawa ushahidi uliopelekea kuamini ufufuko.
Katika sura yake ya kwanza, Kitabu kilichokataa kuandikwa” mkosoaji wa zamani alielezea jinsi gani ushahidi ulimfanya aamini kwamba ufufuko wa Yesu ulikuwa ni tukio la kweli la kihistoria. Ni kama mtu ameamua kukatisha msitu kwa njia ijulikanayo na ghafla akatokeza ambapo hakutegemea kutokeza.”[36]
Morison hayuko peke yake katika hilo. Wakosoaji wengine wasiohesabika wamechunguza ushahidi wa ufufuko wa Yesu na wameukubali kuwa ni ukweli wa kushangaza katika historia zote za binadamu. Lakini ufufuko wa Yesu Kristo umeibua swali: Ni kitu gani ambacho ukweli kwamba Yesu ameshinda kifo kinahusu maisha yangu? Jibu kwa swali hilo ndicho kile Agano Jipya la Ukristu linachohusu.
Ikiwa kweli Yesu alifufuka toka katika wafu, basi ni yeye pekee lazima anajua kitu gani kipo upande mwingine wa kifo. Kitu gani Yesu alisema kuhusu maana ya maisha na siku zetu zijazo? Kuna njia nyingi kwa Mungu au Yesu alidai kuwa njia ya pekee? Soma majibu ya kushangaza kwenye kurasa “Kwanini Yesu”
Yesu anaweza kuleta maana katika maisha?
“Kwanini Yesu” inaangalia katika swali la kwamba Yesu anahusika au hahusiki leo. Je Yesu anaweza kujibu maswali makubwa ya maisha: “Mimi ni nani?” “Kwanini nipo hapa?” na “NInakwenda wapi?” Makanisa yaliyokufa na misalaba yamepelekea kwa baadhi kuamini kwamba hawezi, na kwambwa Yesu ametuacha kukabiliana na dunia iliyo bila nguvu ya kuitawala. Lakini Yesu ameweka madai kuhusu maisha na madhumuni yetu hapa duniani kwamba yanahitaji kuchunguzwa kabla hatujamtupa kuwa hafai au hana manufaa. Makala hii inachunguza siri za kwani Yesu alikuja duniani.
Bonyeza hapa kusoma “Kwanini Yesu” na kugundua nini Yesu alisema juuya maisha baada ya kifo.
« Previous | Next »