Kifo cha Kutisha na kisha…?
Unajua zile saa za mwisho za Yesu za maisha ya duniani zilivyokuwa, iwapo uliangalia sinema ya mpiganaji wa njiani, shujaa Mel Gibson. Iwapo ulikosa kuona sehemu za Upendo wa Kristo kwa sababu ulikinga macho yako (ingekuwa rahisi kuchukua sinema na kichujio chekundu kwenye kamera) na kufungua kurasa za nyuma za Injili yoyote katika Agano Jipya lako kujua kilichokosekana.
Kama Yesu alivyotabiri, alisalitiwa na mmoja wa wafuasi wake, Yuda Iscariot, na alikamatwa. Katika shitaka la kufedhehesha chini ya Gavan wa Kirumi, Pontio Pilato, alitiwa hatia ya uhaini na alilaaniwa kufa kwenye msalaba wa mbao. Kabla ya kupigiliwa misumari msalabani, Yesu alipigwa kwa ukatili kwa mjeledi wenye mifupa vyuma ambao ulinyofoa nyama. Alisukumwasukumwa, alipigwa mateke, na alitemewa mate.
Kisha, wakitumia nyundo, watesaji wa Kirumi walipigilia misumari mizito ya chuma kwenye kitanga cha mkono na miguu. Mwishowe waliudumbukiza msalaba kwenye shimo ardhini kati ya wezi wengine waliobeba misalaba.
Yesu alining’inia pale kwa saa karibia sita. Kisha mnamo saa 9:00 alasiri, yaani mnamo muda ule ule ambao mwanakondoo wa Pasaka alikuwa akitolewa sadaka kama matoleo ya dhambi (kuna ujumbe fulani hapo, umeuona?) Yesu alilia, “Yamekwisha” (kwa kiAramaiki) na akafa. Ghafla, anga likawa giza na tetemeko la radhi likaitikisa dunia.[9]
Pilato alitaka uthibitisho kwamba Yesu alikuwa amekufa kabla ya kuruhusu mwili wake uliosulubiwa kuzikwa. Kwa hiyo mlinzi wa kirumi, alisukuma mkuki katika ubavu wa Yesu. Mchanganyiko wa damu na maji ambao ulitiririkia nje ulikuwa ni ishara tosha kwamba Yesu alikuwa amekufa. Mwili wa Yesu kisha ulichukuliwa toka msalabani na kuzikwa kwenye kaburi la Yosefu wa Arimathea. Walinzi wa kirumi kisha wakaliziba kaburi na wakalilinda kwa saa.
Wakati huo huo, wafuasi wa Yesu walikuwa katika mshtuko. Dk. J. P. Moreland anaeleza jinsi gani walivyofadhaishwa na walivyochanganyikiwa baada ya kifo cha Yesu msalabani. “Hawakuwa tena na ujasiri kwamba Yesu alikuwa ametumwa na Mungu. Pia walifundishwa kwamba Mungu asingeruhusu Masiha wake atesekee mauti. Hivyo walitawanyika. Harakati kwa ajili ya Yesu zilikuwa zimekwisha simama katika njia zake.”[10]
Matumaini yote yalikwisha. Roma na viongozi wa kiyahudi waliendelea – kama hivyo ilivyoonekana.