Je, Yesu kudai kuwa ni Mungu wa Ibrahimu naMusa?
Yesu aliendelea kujiita katika namna ambazo ziliwastaajabisha wasikiliza wake. Kama ambayo Piper alivyonukuu, Yesu alitoa kauli za kujiamini, “Kabla ya Abraham kuweko, MIMI NIPO.[11] “Alimwambia Martha na wengine waliomzunguka, “MIMI NI ufufuo na uzima;[12] yeyote aniaminiye, japo amekufa, ataishi”[13] “MIMI NI njia pekee ya uzima”[14] au, “Mimi ni kweli”[15] Haya na mengine kadhaa ya madai yake yalitanguliwa na maneno matakatifu kwa ajili ya Mungu, “MIMI NI (ego eimi).[16] Yesu alimaanisha nini kwa hizo kauli, nini maana na umuhimu wa neno “MIMI NI”?
Kwa mara nyingine, lazima turejee kwenye maudhui. Katika maandiko ya kiebrania, wakati Musa alipomwomba Mungu kwa jina lake katika kichaka kiwakacho, Mungu alijibu “MIMI NI”. Alikuwa akijidhihirisha kwa Musa kwamba yeye ni Mungu moja wa pekee ambaye yuko zaidi ya nyakati na aliyekuwapo sikuzote. Kwa kiasi kikubwa Yesu alikuwa akitumia maneno haya matakatifu kujielezea yeye. Swali ni “Kwanini?”
Tangu kipindi cha Musa, hakuna myahudi angejiita mwenyewe au kitu chochote kwa kutumia “MIMI NI”. Kama yalivyokuwa matokeo, Madai ya Yesu ya “MIMI NI” yaliwakasirisha viongozi ya kiyahudi. Wakati mmoja kwa mfano, baadhi ya viongozi walieleza kwa Yesu kwanini walikuwa wanajaribu kumuua. “Kwa sababu, wewe mtu tu umejifanya mwenyewe kuwa Mungu.”[17]
Matumizi ya Yesu ya jina la Mungu, yaliwakasirisha kwa kiasi kikubwa viongozi wa dini. Pointi ni kwamba hawa wasomi wa Agano la Kale, walijua hasa nini alikuwa akisema – alikuwa akidai kuwa Mungu, kwa uwazi imedhihirika, si kwa kwa maneno yake tu, lakini pia kwa hatua hasi zao kwa maneno hayo.
C. S. Lewis mwanzo alimfikiria Yesu kuwa hadithi. Lakini msomi huyu mwerevu, aliyezijua hadithi vizuri, alihitimisha kwamba Yesu alikuwa mtu kweli. Zaidi ya hapo, wakati Lewis alipokuwa akichunguza uthibitisho wa Yesu, alihakikishiwa kwamba sio tu kwamba Yesu alikuwapo kweli, lakini pia hakuwa kama mtu yeyote aliyeishi. Lewis anaandika,
“Kisha kuna kitu cha kushangaza kweli” Lewis anaandika, “Miongoni mwa hawa wayahudi, hapo ghafla anatokea mtu anayeendelea kuzungumza kama vile alikuwa Mungu. Anadai kusamehe dhambi. Anasema siku zote aliwakuwapo. Anasema atakuja kuhukumu ulimwengu katika siku za mwisho.”[18]
Kwa Lewis, madai ya Yesu yalikuwa makubwa na mazito sana kufanywa na mwalimu wa kawaida au mwalimu wa dini. (Kwa kuangalia kwa undani zaidi madai ya Yesu kuwa Mungu, angalia “Je Yesu alidai kuwa Mungu?” (Saa Kwanini Yesu?)