Uamuzi wa Wasomi
Lakini je, kanisa la kale lingeweza kuharibu ushahidi katika jaribio lao la kuandika upya historia ya Yesu? Bila shaka hicho ndicho kitu Jacobovici, Brown, na kundi la wapiga chuku yaani waandika vioja au wadadisi wengine wanachosema. Lakini wasomi wanakubaliana nacho?
Makala ya gazeti la Newsweek inaandika kwa kifupi maoni ya wasomi yanayoongoza, kwa uwazi yakisema kwamba wazo la Yesu na Maria Magdalena walioana hayana msingi wa kihistoria.[2]Labda wanostiki yaani wazushi wajuaji wachache walifikiri Agano Jipya lilikuwa na aibu kuhusiana na mapenzi na wakaamua kulikoleza suala hilo kidogo. Kwa sababu yoyote ile, aya hizi zilizotengwa na zilizojificha ziliandikwa miaka 100 – 200 baada ya Kristo haziko zaidi katika kuikita nadharia ya hila za njama juu yake. Usomaji wa kuvutia labda, lakini kabisa siyo historia.
Lakini baadhi wanabaki hawaamini. Labda wanataka tu kuifanya historia ivutie zaidi. Mwandishi wa habari za televisheni aliyeshinda tuzo Frank Sesno aliuliza jopo la wasomi wa kihistoria kuhusu tabia ya kuvutiwa na kitu watu waliyo nayo kwa nadharia ya hila za njama. Profesa Stanley Kutler kutoka Chuo Kikuu cha Wisconsin alijibu, “Wote tunapenda matukio ya ajabu ya siri, lakini tunapenda habari za njama zaidi.”[3]
Labda habari zote kuhusu Yesu na Maria zina umuhimu zaidi wa kufanya kwa wapinzani wa ukristu wakijaribu kumfanya aonekane binadamu wa kawaida mtu ambaye wakristu tangu mwanzo wamemwita “Mungu” (Kusoma zaidi kuhusu jinsi gani wakristu wa zamani walimwona Yesu (Angalia saa Tabasamu la MonaLisa). Kwa mfano, mtume Paulo alisema kuhusu Yesu Kristo:
“Ingawa alikuwa Mungu, hakuhitaji na kushikilia hadhi zake kama Mungu. Alijifanya hana kitu, alichukua nafasi ya unyenyekevu ya mtumwa na alionekana katika umbo la kibinadamu” (Wafilipi 2:6, 7a).
Yohana, shahidi wa macho, na mmoja wa wafuasi wa karibu wa Yesu, alimzungumzia hivyo.
“Katika mwanzo neno tayari lilikuwapo. Alikuwa pamoja na Mungu, na alikuwa Mungu… aliumba kila kitu kilichopo… hivyo neno likawa mwanadamu na likaishi hapa duniani miongoni mwetu.”(sehemu za Yohana 1:1-3, 14).
Je ni kweli Yesu alifufuka toka katika Wafu?
Swali kubwa kabisa la wakati wetu si kwamba Yesu na Maria Magdalena walioana, lakini “Nani ni Yesu Kristo wa Kweli?” Alikuwa mtu wa kipekee, au alikuwa Mungu katika mwili, kama Paulo, Yohana, na wafuasi wake wengine walivyoamini?
Mashahidi wa macho kwa Yesu Kristo kwa kweli walizungumza na walitenda kama walivyoamini, aliinuka kimwili toka katika wafu baada ya kusulubiwa kwake. Ikiwa hawakuwa sahihi basi Ukristu umejengwa katika uongo. Lakini kama walikuwa sahihi, muujiza huo ungethibitisha yote Yesu alisema kuhusu Mungu, yeye mwenyewe na sisi.
Lakini lazima tuchukue ufufuko wa Yesu Kristo kwa imani pekee, au kuna ushahidi mzito wa kihistoria? Wakosoaji wachache walianza uchunguzi kwenye rekodi za kihistoria kuthibitisha maelezo ya ufufuko ni uongo. Ni kitu gani waligundua? Saa Yesu Alifufuka Wafu.
Kulikuwa na Hila za Da Vinci ?
“Tabasamu la Monalisa” inachunguza fikra kuhusu njama zinaoongoza duniani kuhusu Yesu Kristo. Je, Yesu na Maria Magdalena waliooana? Je Constantine aliagiza uharibifu wa rekodi za kweli za Yesu Kristo akimwelezea upya kuwa Mungu wakristu wanavyomwabudu leo? Saa Tabasamu la MonaLisa.
Je, Yesu alisema kitu gani kinatokea baada ya sisi kufa?
Ikiwa ni kweli Yesu alifufuka toka katika Wafu, basi lazima ajue kitu gani kipo upande mwingine. Ni kitu gani alisema kuhusu maana ya maisha na siku zetu zijazo? Kuna njia nyingi kwenda kwa Mungu au Yesu alidai kuwa njia pekee? Soma majibu ya kushangaza “Kwanini Yesu?” Saa Kwanini Yesu?
Je, Yesu anaweza kuleta maana katika maisha?
“Kwanini Yesu? inaangalia suala la kwamba Yesu ni muhimu leo. Je, Yesu anaweza kujibu swali kubwa la maisha: “Mimi ni nani?” “Kwanini niko hapa?” na, “Wapi ninaenda?” Makanisa yaliyokufa na misalaba imewaongoza wengine kuamini kwamba hawezi, na kwamba Yesu ametuacha sisi kuendana na dunia iliyo nje isiyo na udhibiti. Lakini Yesu amefanya madai kuhusu maisha na madhumuni yetu hapa duniani ambayo yanahitaji kuchunguzwa kabla hatujamkataa kama asiyejali na asiye na nguvu. Makala hii inachunguza siri ya kwanini Yesu alikuja duniani. Saa www.Kwanini Yesu?
Ni kweli Yesu alifufuka toka katika Wafu?
Mashahidi wa macho kwa Yesu Kristo kwa kweli walizungumza na walitenda kama walivyoamini, alifufuka toka katika wafu baada ya kusulubiwa kwake. Ikiwa walikosea basi uKristu umeanzishwa kwa uongo? Lakini kama walikuwa sahihi, muujiza huo ungethibitisha yote Yesu aliyosema kuhusu Mungu, kuhusu yeye na kutuhusu sisi.
Lakini ni lazima tuamini ufufuko wa Yesu Kristo kwa imani pekee, au kuna ushahidi wowote wa kihistoria? Wakosoaji kadhaa walianza uchunguzi kwenye kumbukumbu za kihistoria kujaribu kuona kama kweli maelezo ya ufufuko yalikuwa uongo. Kitu gani waligundua?
Kuangalia ushuhuda wa madai makuu yaliyowahi kufanyika ya ufufuko wa Yesu Kristo!
Bonyeza hapa kwa ajili ya kudai zaidi fantastic milele alifanya – ya ufufuo wa Yesu Kristo!
« Previous | Next »