Injili ya Maria (Magdalena)
Wazo kwamba Maria Magdalena alikuwa mtu maalum kwa Yesu inachukuliwa hasa kutoka Injili ya Maria. Injili hii ya Kinostiki (Kijuaji) si sehemu ya Agano Jipya, na iliandikwa na mtunzi asiyejulikana katika nusu ya karne ya pili, au karibia miaka mia na hamsini baada ya kifo cha Yesu. Hakuna mashahidi wa macho, akiwamo Maria mwenyewe wangekuwa hai wakati ilipoandikwa (karibia miaka 150 A. D.). Tarehe hiyo ya mwishoni inamaanisha Injili ya Maria haikuandikwa na shahidi wa macho wa Yesu, na hakuna anayejua aliyeiandika.
Aya moja katika Injili ya Maria inamwelezea Maria Magdalena kama mfuasi kipenzi wa Yesu, inasema alimpenda Maria zaidi kuliko sisi (maana yake wafuasi wake)” Katika aya nyingine Peter inavyoaminika alimwambia Maria, Dada, twajua mwokozi alikupenda zaidi ya mwanamke mwingine yeyote” Lakini hakuna kilichoandikwa katika Injili ya Maria kinachozungumzia mapenzi au uhusiano wa kimapenzi kati ya Maria Magdalena na Yesu.
Injili ya Philipo
Maandiko ya Da Vinci yameweka dai lake kwamba Yesu na Maria walikuwa wameoana na walikuwa na mtoto kwenye aya moja pekee katika Injili ya Kinostiki (Kijuaji) ya Philipo ambayo inaonesha Yesu na Maria walikuwa marafiki. Aya hii inasema: (Mabano yanaonekana ambapo maneno ya andiko yanakosekana au hayasomeki)
“Wanawake watatu siku zote walitembea na BWANA: Maria mama yake, dada na Maria Magdala ambaye aliitwa mwenzi wake. Kwa “Maria” ni jina la dada yake, mama yake na mwenzi/rafiki wake”
In mtaalamu wa Maandiko ya kubuni ya Da Vinci, Sir Leigh Teabing anasema kwamba neno kwa neno rafiki lingeweza kumaanisha mwenzi. Lakini kulingana na wasomi, hiyo ni tafsiri isiyoelekea. Kwa kuanza, neno kwa ujumla lililotumika kwa mke katika Agano Jipya Kigiriki ni “gune” sio “koinonos” Ben Witherington III, akiandika katika Rejea ya Kibiblia ya Elimu-Kale, alizungumzia pointi hii muhimu:
“Kulikuwa na neno lingine la Kigiriki, gune, ambalo lingeweka neno hili wazi. Ni kama neno koinonos hapa linamaanisha “dada” katika maana ya kiroho kwa sababu hivyo ndivyo linavyotumika mahali pengine pote katika aina hii ya uandishi. Katika hali yoyote, maandishi haya hayasemi waziwazi wala kudokeza kwamba Yesu alikuwa amemuoa Maria Magdalena.”[1]
Kuna aya moja pia katika Injili ya Philipo ambayo inasema Yesu alimbusu Maria.
“Mwenzi ni Maria wa Magdala. Alim… yeye zaidi ya wafuasi, alimbusu yeye mara nyingi kwenye. Mwingine …alimwambia, ‘Kwanini unampenda yeye zaidi kuliko sisi sote?’”
Kuwasalimia marafiki kwa busu kulikuwa kawaida katika karne ya kwanza, na hakukuwa na ishara ya mapenzi. Profesa Karen King anaeleza kwenye kitabu chake Injili ya Maria Magdala, kwamba busu katika maandiko ya Philipo hasa ilikuwa ni busu safi lisilo la mapenzi bali la ushirika/umoja.
Lakini labda muhimu zaidi ni ukweli kwamba Injili ya Philipo iliandikwa na mtunzi asiyejulikana karibu miaka 200 baada ya maelezo ya mashahidi wa macho wa Agano Jipya (Angalia saa Andiko la Yesu na saa Tabasamu la MonaLisa.
Ni muhimu pia kufahamu kwamba, mbali ya hivi vifungu vichache kwa kuulizwa, hakuna andiko lingine la kihistoria ambalo linadokeza Yesu na Maria walikuwa na uhusiano wa kimapenzi. Hakuna mwanahistoria wa kawaida, au mwanahistoria wa kikristu aliyeandika hata robo kuhusu uhusiano huo. Na kwa sababu Injili zote, Injili ya Maria na Injili ya Philipo ziliandikwa miaka 100 – 220 baada ya Kristo na watunzi wasiojulikana, maelezo yao kuhusu Yesu na Maria yanahitaji kutathminiwa katika mazingira yote ya historia ya wakati ule na maandiko ya mwanzoni kabisa ya Agano Jipya.