Yesu ni nani Halisi?

Ukweli kuhusu Yesu Kristo.

  • Kiingereza Home
  • Swahili Home
  • Kutuma Maoni

Injili za Siri: Kuna maandiko ya siri kuhusu Yesu?

Kosozi za mwanzo

Mazoea kidogo ya falsalfa za siri za wachache yalikuwa tayari yanakua katika karne ya kwanza, miongo kadhaa ya kifo cha Yesu. Mitume katika mafundisho na maandiko yako, walienda mbali kulaumu imani hizi kwamba zimepingana na ukweli wa Yesu, kwake yeye ambaye walikuwa mashahidi wa macho.

Angalia, kwa mfano, kile mtume Yohana aliandika karibu mwisho wa karne ya kwanza:

Nani ni mwongo mkubwa? Anayesema kwamba Yesu si Kristo. Watu hao ni wapinga Kristo, kwa sababu wamemkana Baba na Mwana. (1 Yohana 2:22, NIV).

Wakifuata mafundisho ya mitume, viongozi wa kanisa la mwanzo kwa pamoja wakalaumu mafundisho ya Kinostiki ya siri ya wachache kuwa ni ya kidhehebu-tenge. Padri wa Kanisa Irenaeus, akiandika miaka 140 kabla ya Baraza la Nicaea, alihakikisha kwamba Wanostiki walilaumiwa na kanisa kama wapinzani. Pia alizikataa “injili” zao. Vile vile, akirejelea kwenye Injili nne za Agano Jipya, alisema, “Haiwezekani kwamba Injili zinaweza kuwa zaidi au chache kwa idadi kuliko zilivyo.”[2]

Mwanateolojia Origen aliandika hili katika karne ya tatu, zaidi ya miaka mia moja kabla ya Nicaea:

Najua injili fulani ambayo inaitwa “Injili kulingana na Thomaso” na “Injili kulingana na Mathayo”, na nyingi nyinginezo tulizosoma – tusifikiriwe kwa njia yoyote wajinga kwa sababu ya hao wanaofikiri wanamiliki elimu fulani ikiwa wamejulishwa haya.

Hata hivyo, miongoni mwa yote haya tuliyothibitisha pekee ambayo kanisa limetambua, ambalo ni kwamba Injili nne tu zinapaswa kukubaliwa.[3]

Watunzi wa Siri

Inapokuja kwenye injili za siri za wachache, karibu kila kitabu kinabeba jina la sifa ya Agano Jipya: Injili ya Philipo, Injili ya Petro, Injili ya Maria, Injili ya Yuda, na kuendelea . Lakini ziliandikwa na watunzi wao waliokusudia? Hebu tuangalie.

Injili za Wanostiki zinawekewa tarehe karibia miaka 100 hadi 300 baada ya Kristo, hakuna msomi wa kuaminika anaamini chochote kati ya hivyo ambavyo vingeweza kuandikwa na wenzi-jina (somo) wao. Katika maktaba ya James M. Robinson’s Maktaba ya Nag Hammadi tunajifunza kwamba Injili za Kinostiki za wachache ziliandikwa hasa kwa kiasi kikubwa na watunzi wasiojulikana wasiohusiana.[4]

Msomi wa Agano Jipya Norman Geisler anaandika “Maandiko ya Siri ya Wachache (Wanostiki) hayakuandikwa na mitume, bali na watu katika karne ya pili (na baadaye) wakijifanya kutumia mamlaka ya kitume kuendeleza mafundisho yao wenyewe. Leo tunaita suala hili uongo na uzushi wa kufoji.”[5]

« Previous | Next »

Pages: 1 2 3

Yesu ni nani Halisi?

  • Yesu Alikuwa mtu Kweli?
  • Kulikuwa na Hila za Da Vinci?
  • Yesu ni Mungu?
  • Injili ni za Kweli?
  • Yesu Alikuwa Masiha?
  • Je, Yesu Alifufuka toka Katika Wafu?
  • Yesu ni Muhimu Leo?

MASWALI ZAIDI KUHUSU YESU

  • Yesu na Maria Magdalena: Walikuwa na ndoa ya siri?
  • Injili za Siri: Kuna maandiko ya siri kuhusu Yesu?
Copyright © 2023 - JesusOnline
Menu
  • Yesu Alikuwa mtu Kweli?
  • Kulikuwa na Hila za Da Vinci?
  • Yesu ni Mungu?
  • Injili ni za Kweli?
  • Yesu Alikuwa Masiha?
  • Je, Yesu Alifufuka toka Katika Wafu?
  • Yesu ni Muhimu Leo?
  • Yesu na Maria Magdalena: Walikuwa na ndoa ya siri?
  • Injili za Siri: Kuna maandiko ya siri kuhusu Yesu?