Hii inatuleta kwenye suala la pili; kwani injili hizi za kiroho za siri ziliharibiwa na kuondolewa toka katika Agano Jipya? Ndani ya kitabu, Teabing anadai kwamba maandiko ya siri yaliondolewa toka katika Biblia 50 zilizoidhinishwa ikisimamiwa na Constantine katika Baraza. Alimwambia Neveu kwa shauku:
“Kwa sababu Constantine alikweza hadhi ya Yesu karibia karne nne baada ya Kifo cha Yesu, maelfu ya maandiko tayari yalikuwapo yakiandika maisha yake kama mtu tu. Kuandika tena historia ya vitabu, Constantine alijua angehitaji kitendo cha kishujaa. Kutoka katika hili pakajitokeza wakati muhimu katika historia ya Kikristo.”[7]
Constantine akaamuru na akafadhili Biblia mpya ambayo iliondoa hizo injili ambazo zilizungumzia sifa/tabia pambanishi za kibinadamu za Kristo na akapamba injili hizo ambazo zilimfanya yeye kama Mungu. Injili za mwanzo zilitanguliwa, zikakusanywa na zikachomwa moto.
Je, haya maandiko ya wachache ya siri yalikuwa ni historia ya kweli ya Yesu Kristo? Ngoja tuangalie kwa kina tuone kama tunaweza tenganisha ukweli kutoka kwa kubuni.
“Wajuaji” wa siri
Injili za siri za wachache zinaunganishwa kwenye kundi lijulikanalo kama (shangazo kuu hapa) Elimu ya Siri. Jina lao linatoka katika neno la kigiriki, gnosis, likimaanisha “maarifa” Watu hawa walifikiri wana siri, maarifa maalumu yaliyofichwa mbali na watu wa kawaida.
Kati ya maandiko 52, matano tu yaliorodheshwa kama injili. Kama tutakavyoona, hizi ziitwazo injili zinatofautishwa toka katika Injili za Agano Jipua, Mathayo, Mark, Luka na Yohana.
Kama Ukristu ulivyoenea, ujuzi ulichanganya baadhi ya imani na masuala ya ukristu katika imani zao wakichanganya ujuzi kwenye Ukristu bandia. Labda walifanya hivyo kuongeza idadi ya kuajiri na kumfanya Yesu mtoto wa matangazo kwa sababu zao. Pia, ili utaratibu wao wa fikra uweze kuendana na Ukristu, Yesu alihitaji kuwa kuelezewa upya, akavuliwa wote ubinadamu wake na utakatifu wake halisi.
Katika Historia ya Ukristu ya Oxford, John McManners aliandika mchanganyiko wa elimu siri wa ukristu na imani za kubuni za uongo.
“Ujuzi-siri ulikuwa (na bado ni) theosophia (elimu ya Mungu ya kiroho) zenye michanganyiko mingi. Ushirikina na imani za uongo za kienyeji zilichanganywa na elimu ya nyota, uchawi. … wakakusanya misemo ya Yesu iliyotengenezwa kufaa tafsiri zao (kama katika Injili ya Thomaso), na wakawapa wafuasi wao fursa au namna ya upinzani wa Ukristu .”[8]