Kumtukuza Yesu
Ili kujibu madai ya Brown, lazima kwanza tutambue kitu gani wakristo kwa ujumla waliamini kabla Constantine hajaitisha mkutano wa Halmashauri ya Nicaea.
Wakristu wamekuwa wakimwabudu Yesu kama Mungu tangu karne ya kwanza. Lakini katika karne ya nne, kiongozi wa kanisa kutoka mashariki, Arius, alianzisha kampeni kulinda utakatifu-mmoja wa Mungu. Alifundisha kwamba Yesu aliumbwa mahususi mkuu kuliko malaika, lakini si Mungu. Athanazi na viongozi wakuu wa kanisa kwa upande mwingine, walisadikishwa kwamba Yesu alikuwa ni Mungu katika mwili.
Constantine alitaka kusuluhisha mzozo huo, akitumaini kuleta amani katika himaya yake, akiunganisha migawanyiko ya mashariki na magharibi. Hivyo mwaka 325 A.D., aliita zaidi ya maaskofu 300 katika Nicaea (ambayo kwa sasa ni sehemu ya Uturuki) toka katika dunia yote ya Ukristu. Suala nyeti ni, je kanisa la mwanzo lilifikiria Yesu alikuwa Muumbaji au tu ni uumbaji – mwana wa Mungu au mwana wa mseremala? Hivyo, ni kitu gani manabii walifundisha kuhusu Yesu? Kutoka katika kauli za mwanzo kabisa zilizorekodiwa, zilimchukulia kama Mungu. Karibu miaka 30 baada ya kifo na ufufuko wa Yesu, Paulo aliandika kwa Wafilipi kwamba Yesu alikuwa ni Mungu katika umbo la kibinadamu (Wafilipi 2:6-7, NLT). Na Yohana, shahidi wa macho wa karibu, anahakikisha utakatifu wa Yesu katika kifungu kifuatacho:
Hapo mwanzo Neno tayari lilikuwapo. Alikuwa na Mungu, na alikuwa Mungu. Aliumba kila kitu hapo kilipo Hakuna chochote kilichopo ambacho hakukiumba. Uhai/Maisha yenyewe yalikuwa ndani yake, hivyo Neno akawa mwanadamu na akaishi hapa duniani kwetu sisi (Yohana 1: 1-4, 14, NLT).
Kifungu toka kwa Yohana 1, kimevumbuliwa katika maandishi ya kale, na kimewekewa tarehe ya kaboni mnamo 175-225 A.D. Hivyo Yesu kwa uwazi alizungumziwa kama Mungu zaidi ya miaka mia moja kabla ya Constantine hajaitisha mkutano na Baraza la Nicaea. Sasa tunaona kwamba ushahidi wa maandishi wa kisayansi unapinga madai ya maandishi ya Da Vinci kwamba Utakatifu wa Yesu ulikuwa ni uvumbuzi wa karne ya nne. Lakini nini historia inatuambia kuhusu Baraza la Nicaea? Brown anadai katika kitabu chake kupitia kwa Teabing, kwamba wengi wa maaskofu Nicaea walilazimisha imani ya Arius kwamba Yesu alikuwa “mtume wa siku zote” na wakachukua imani ya utakatifu wa Yesu kwa kura ya karibu kiasi.” Uongo au kweli?
Kwa ukweli, kura ilikuwa ya ushindi mkubwa; wawili tu kati ya maaskofu 318 walipinga. Ambapo Arius aliamini kwamba Baba peke yake alikuwa Mungu, na kwamba Yesu alikuwa kiumbe chake kikuuu, Baraza lilihitimisha kwamba Yesu na Baba walikuwa wa asili sawa ya utakatifu mtakatifu.
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu walionekana kuwatofauti, walikuwa pamoja, wadumuo milele kwa pamoja, lakini Mungu mmoja. Imani ya Mungu mmoja katika nafsi tatu ikapata kujulikana kama imani ya Nicene, na ni msingi mkuu wa Imani ya Kikristo. Sasa, si kweli kwamba Arius alikuwa mshawishi na alikuwa na ushawishi mkubwa. Kura ya ushindi mkubwa ikafuatia baada ya majadiliano mazito. Lakini mwishoni mwa Baraza kwa kushinda kwa nguvu likatangaza Arius kuwa mpinzani kwa sababu mafundisho yake yanapingana na kile mitume walikuwa wakifundisha kuhusu utakatifu wa Yesu.
Historia pia inakikisha kwamba Yesu aliruhusu kwa waziwazi kuheshimiwa alikopokea toka kwa wafuasi wake. Na, kama tulivyoona, Paulo na mitume wengine kwa wazi walifundisha kwamba Yesu ni Mungu na anastahili kuabudiwa.
Tangu siku za kwanza za Kanisa la Kikristo, Yesu alichukuliwa zaidi ya mtu wa kawaida, na wengi wa wafuasi wake walimwabudu yeye kama Bwana-Muumbaji wa ulimwengu. Hivyo, jinsi gani Constantine awe amebuni imani ya utakatifu wa Yesu ikiwa kanisa lilishamchukulia Yesu kama Mungu kwa zaidi ya miaka 200? Maandiko ya Da Vinci hayaelezei suala hili.