Kushambulia Kitabu cha Dini
Maandishi ya Da Vinci pia yanaeleza kwamba Constantine alikandamiza/ficha maandiko yote yamhusuyo Yesu zaidi ya hayo yaliyopatikana katika Agano Jipya letu la sasa (yaliyotambuliwa na kanisa kama ripoti za ushahidi halisi wa macho za mitume. Inadaiwa zaidi kwamba maelezo ya Agano Jipya yalibadilishwa na Constantine na maaskofu kumwelezea Yesu upya. Suala lingine la msingi lala ushiriki wa maandiko ya Da Vinci ni kwamba injili nne za Agano Jipya ziliteuliwa toka katika jumla ya zaidi ya injili 80, nyingi kati ya hizo inasadikiwa zilifichwa na Constantine.[5]
Kuna masuala makuu mawili hapa, na tunahitaji kuyashughulikia yote. La kwanza ni kwamba je Constantini alibadilisha au alipendelea uteuzi wa Vitabu vya Agano Jipya. La pili ni kwamba alizuia maandiko ambayo yangejumuishwa katika Biblia.
Tukitazama suala la kwanza, barua na maandiko yaliyoandikwa na viongozi wa kanisa wa karne ya pili na wapinzani vile vile wanahakikisha matumizi makubwa ya vitabu vya Agano Jipya. Karibu miaka 200 kabla ya Constantine hajaita Baraza la Nicaea, mpinzani Masioni aliorodesha 11 kati ya 27 ya vitabu vya Agano jipya kama maandiko halisi ya mitume.
Na karibia wakati huo huo, mpinzani mwingine, Valentinus, anagusia katika aina nyingi mbali mbali za vifungu na ujumbe wa Agano Jipya. Kwa sababu wapinzani wawili walikuwa wapinzani uongozi wa kanisa wa zamani za mwanzo, hakuwa wanaandika kile maaskofu walitaka. Lakini kama ilivyokuwa kwa kanisa la kale, bado walirejelea katika vitabu vya Agano Jipya tusomavyo leo.
Hivyo, ikiwa Agano Jipya tayari lilikuwa katika matumizi miaka 200 kabla ya Constantine na Baraza la Nicaea, ni jinsi gani mtawala angeweza kulibuni na kulibadili? Kabla ya wakati huo kanisa lilikuwa limeshaenea na kukusanya mamia ya maelfu kama siyo mamilioni ya waamini, wote walikuwa wanafahamu maelezo ya Agano Jipya.
Katika kitabu chake, Ulaghai wa Da Vinci,, upembuzi wa Maandishi ya Da Vinci, Dk. Erwin Lutzer anasema,
“Constantine hakuamua vitabu gani viwemo katika orodha rasmi ya dini, pia mada ya orodha rasmi ya vitabu vya dini haikujitokeza katika Baraza la Nicaea. Kabla ya wakati huo, kanisa lilikuwa likisoma orodha rasmi ya vitabu vya dini ambayo ilikuwa imehakikisha ilikuwa ni Neno la Mungu miaka mia mbili kabla.”[6]
Ingawaje orodha rasmi ilikuwa bado miaka kabla haijahitimishwa, Agano Jipya la leo lilionekana rasmi zaidi ya karne mbili kabla ya Nicaea.