Je, wafuasi walikuwa wanaona mizuka?
Watu bado wanafikiri wanamwona Elvis, mnene, mwenye nywele za kijivu akingia kenye Donati za Dunkin. Na kuna hao ambao wanaamini waliutumia usiku wa jana pamoja na viumbe toka mbali katika meli ambavyo ni havielezeki kiupimaji. Nyakati fulani watu fulani wanaweza kuona vitu wanavyotaka kuona, vitu ambavyo havipo kweli. Na ndio maana baadhi wamedai kwamba wafuasi walifadhaishwa sana na kusulubishwa kiasi kwamba hamua yao ya kumuona Yesu hai ilisababisha kuota ndoto za mchana, kuona vitu visivyokuwapo. Inaiingia akilini?
Mwanasaokolojia Gary Collins, raisi wa zamani wa Washauri wa Chama Wakristu cha Marekani, aliulizwa uwezekano kwamba maluweluwe yalikuwa kwa wafuasi na ndiyo yaliyobadili kwa kiasi kikubwa tabia yao. Collins alieleza, “Maluweluwe ni matukio ya mtu mmoja mmoja pekee” Kwa asili yake ni mtu mmoja peke yake anaweza kuona luweluwe fulani kwa wakati mmoja. Kwa hakika si vitu ambavyo vinaweza kuonwa na kikundi cha watu kwa wakati mmoja.”[28]
Maluweluwe si uwezekano wa kuona kitu cha mbali, kulingana na mwanasaikolojia Thomas J. Thorbum. “Haiingii akilini kabisa kwamba … watu mia tano, wenye akili timamu za kawaida wawe wameona aina zote za fahamu, za kuona, kusikia, kutenda – na kwamba zote hizi fahamu ziwe zimetokana na kuona maluweluwe – ndoto za mchana!”[29]
Licha ya hayo, katika saikolojia ya maluweluwe, mtu anahitaji kuwa katika mazingira ya akili ambapo walihitaji sana kuona mtu huyo ambaye akili yao iliitayarisha. Viongozi wakuu wawili wa kanisa la mwanzo, James na Paulo, wote wawili walikutana na Yesu aliyefufuka, hawakutarajia wala kutumainia kwa kujifurahisha. Mtume Paulo, kwa kweli ndiye aliyeongoza mateso ya wakristu, na kubadilika kwake kumebaki kuwa tofauti isiyoelezeka kwa ushuhuda wake binafisi kwamba Yesu alijitokeza kwake amefufuka.
Kuanzia kwenye uongo hadi kuwa simulizi
Baadhi ya wakosoaji wasioamini wanaelezea ufufuko kama ni hadithi iliyokuwa kweli ambayo ilianza na mtu mmoja au zaidi wakidanganya or wakifikiri walimwona Yesu. Kwa muda hadithi ingekuwa na ingezidishwa ukweli kwa kadri ilivyokuwa ikirithishwa. Katika dhana hii, ufufuko wa Yesu inalingana na meza ya duara ya King Arthur, kushindwa kwa George Washington kusema uongo, na ahadi kwamba usalama wa jamii utakuwa suluhisho wakati tutakapouhitaji.
Lakini kuna matatizo matatu makuu kwenye hiyo nadharia.
- Hadithi mara chache huendelea wakati mashahidi kadhaa wanapokuwa hai kuzikanusha. Mwanahistoria mmoja wa Rumi na Ugiriki ya zamani, A.N. Sherwin-White, alidai kwamba habari za ufufuko zilienea kwa haraka kwa muda mfupi na haziwezi kuwa hadithi.[30]
- Hadithi huendelea kwa jadi simulizi na haziji na maandiko ya kihistoria ambayo yanayaweza kutihibitishwa. Lakini Injili iliandikwa ndani ya miongo mitatu ya ufufuko.[31]
- Nadharia ya hadithi, huwa haielezi vya kutosha ukweli wa kaburi lilivyoachwa tupu, au ujasiri wa imani uliohakikishwa kihistoria wa mitume kwamba Yesu alikuwa hai.[32]