Vile vile mwanzo hadi mwisho
Kama vile ripoti za mashahidi hazikutosha kuuhoji ukosoaji wa Morison, alishangazwa pia na tabia ya wafuasi. Ukweli wa historia ambao umewachanganya wanahistoria, wanasaikolojia na wakosoaji vile vile ni kwamba hawa wafuasi 11 ambao mwanzo walikuwa waoga, ghafla walikuwa tayari kukabiliana na udhalilishaji, mateso na kifo. Wote isipokuwa mmoja wa wafuasi wa Yesu walichinjwa kama wafia dini. Wangefanya hivyo kwa uongo, wakijua wameuchukua mwili?
Wahanga wa kiislamu wa mwezi Septemba tarehe 11, walihakikisha kwamba wengine watakufa kwa uongo kwa sababu wanauamini. Lakini kuwa mhanga tayari kufa kwa uongo ni uwendawazimu. Kama ambayo Paulo alivyoandika, “Wanaume watakufa kwa kile wanachoaamini kuwa kweli, ingawaje kinaweza kuwa uongo. Hata hivyo hawafi kwa kile wanachojua ni uongo.”[24] Wafuasi wa Yesu walienenda katika namna iliyoendana na imani kwamba kiongozi wao alikuwa hai.
Hakuna mtu alielezea vya kutosha kwanini wafuasi wangekuwa tayari kufa kwa uongo ulio wazi. Lakini hata kama wangeshirikiana kudanganya kuhusu ufufuko wa Yesu, wangewezaje kuendeleza mpango huo kwa miongo bila hata mmoja wao kuuza siri kwa fedha au madaraka? Moreland aliandika, Hao wanaodanganya kwa faida binafisi hawaendelei kwa muda mrefu hasa wakati shida inapozidi manufaa.”[25]
Msuluhisho wa mizozo wa zamani wa enzi ya utawala wa Nixon, Chuck Colson, aliyekuwamo katika kashifa ya Watergate, alieleza ugumu wa watu kadhaa kuendeleza uongo kwa muda mrefu.
“Najua ufufuko ni ukweli, na Watergate imehakikisha hivyo kwangu. Namna gani? Kwa sababu watu 12 wametoa ushahidi kwamba wamemuona Yesu amemefuka toka katika wafu, na kisha wakatangaza ukweli huo kwa miaka 40, hata mara moja hawajakanusha. Kila mmoja alipigwa, aliteswa, alipigwa mawe na aliwekwa gerezani. Wasingeendeleza hilo kama ingekuwa si kweli. Watergate ilihusisha watu 12 wenye nguvu duniani na hawakuweza kutunza uongo kwa wiki tatu. Unaniambia mitume 12 waliweza kutunza uongo kwa miaka 40? Haiwezekani kabisa.”[26]
Kitu fulani kimetokea ambacho kimebadili kila kitu kwa wanawame na wanawake. Morison alikubali, “Yeyote anakutana na hili tatizo, muda mfupi au baadaye sharti akabiliane na ukweli ambayo hauwezi kuelezewa mbali… ukweli huu ni kwamba…uhakika hasa ulianzia kwa kikundi kidogo cha watu – hatua ambayo inaonesha ukweli kwamba Yesu alifufuka toka kaburini.”[27]