Wizi wa Kaburi?
Wakati Morison akiendelea na uchunguzi wake, alianza kuchunguza msukumo wa wafuasi wa Yesu. Labda ufufuko unaofikiriwa ulikuwa ni mwili ulioibiwa. Lakini kama ni hivyo, jinsi gani mtu anaweza kueleza kuonekana kote kwa Yesu aliyefufuka? Mwanahistoria Paul Johnson katika Historia ya Wayahudi, aliandika, “Kilichokuwa cha muhimu si mazingira ya kifo chake lakini ukweli kwamba aliaminiwa sehemu kubwa na kwa dhati na umati mkubwa wa watu kuwa amefufuka.”[20]
Kaburi lilikuwa tupu kabisa. Lakini haikuwa kutokuwapo mwili tu ambako kungewatia nguvu wafuasi wa Yesu (hasa ikiwa walikuwa ndio hao waliouiba) Kitu fulani cha ajabu kimetokea, kwa wafuasi wa Yesu kuacha kuomboleza, kuacha kujificha, na wakaanza bila kuogopa kutangaza kwamba wamemuona Yesu akiwa hai.
Kila maelezo ya shahidi wa macho yanaripoti kwamba Yesu alionekana kijasiri kwa wafuasi wake, wanawake kwanza. Morison alishangaa kwanini mahasidi wake wangewafanya wanawake kuwa sehemu ya mpango wao. Katika karne ya kwanza, wanawake sanasana walikuwa hawana haki, utu, au hadhi. Ili mpango ufanikiwe, Morison alitoa sababu kwamba, mahasidi wangeelezea wanaume, sio wanawake, kuwa wa kwanza kumuona Yesu hai. Na bado tunasikia kwamba wanawake walimgusa, walizungumza pamoja naye, na walikuwa wa kwanza kuona kaburi tupu.
Baadaye, kulingana na maelezo ya mashahidi, wafuasi wote walimuona Yesu katika zaidi ya matukio kumi tofauti. Waliandika kwamba aliwaonesha mikono na miguu yake na aliwaambia wamguse. Na aliripotiwa kula pamoja nao na baadaye alionekana hai kwa zaidi ya wafuasi 500 katika wakati mmoja.
Mwanafunzi wa sheria John Warwick Montgomery alieleza, “mwaka 56 A.D. [Mtume Paulo aliandika zaidi ya watu 500 walimuona Yesu aliyefufuka na kwamba wengi wao walikuwa bado hai (1 Wakorintho 15:6 ) Inapita mipaka ya uwezo wa kawaida kwamba wakristu wa mwanzo wangetunga hadithi hii na kuihubiri miongoni mwa hao ambao wangeikana kirahisi kwa kuufichua mwili wa Yesu.”[21]
Wanafunzi wa Biblia Geisler na Turek wanakubali, “Ikiwa ufufuko haukutokea, kwani Mtume Paulo atoe orodha hiyo ya mashahidi waliofikiriwa? Angepoteza heshima yote kwa viongozi wakorintho kwa kudanganya waziwazi kwa makusudi.”[22]
Petro aliwaambia watu Kaisari kwanini yeye na wafuasi wengine waliamini Yesu alikuwa hai.
Sisi mitume ni mashahidi wa yote aliyofanya Israel na Yerusalem. Walimuua kwa kumsulubu, lakini Mungu alimwinua hai siku tatu baadaye… Sisi tulikuwa hao tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya kufufuka toka katika wafu (Matendo 10: 39 – 41)
Mwanafunzi wa Biblia mwingereza Michael Green alisema, “Kuonekana kwa Yesu kunahakikishwa kama kitu kingine chochote hapo kale…. Hakuna shaka kabisa kwamba ilitokea.”[23]