Suala la Kaburi Tupu
Hakuna mwanahistoria wa kweli anatia shaka Yesu alikuwa amekufa wakati alipochukuliwa toka msalabani. Vile vile, wengi wameuliza jinsi gani mwili wa Yesu ulivyoweza kutoweka kaburini. Mwandishi Mwingereza, Dr. Frank Morison, mwanzo alidhania ufufuko ulikuwa ni hadithi au danganya-toto, and alianza utafiti kuandika kitabu kuukataa.[17]Kitabu kikawa maarufu lakini kwa sababu zingine tafauti na kusudio lake la mwanzo, kama ambavyo tutaona.
Morison alianza kwa kujaribu kuchunguza suala la kaburi kuwa tupu. Kaburi lilikuwa mali ya mwanachama wa Halmashauri ya Sanhedrini, Yosefu wa Arimathayo. Nchini Israel katika wakati huo, kuwa katika Halmashauri ilikuwa ni kama kuwa mtu-nyota maarufu. Kila mtu alijua nani alikuwa katika Halmashauri. Yosefu lazima alikuwa ni mtu halisi wa ukweli. Vinginevyo, viongozi wa kiyahudi wangeweka wazi habari hii kuwa ni uongo katika jaribio lao la kukana ufufuko. Pia kaburi la Yosefu lingekuwa katika sehemu inayojulikana na kutambulika kwa urahisi, hivyo mawazo yoyote ya kuwa Yesu alipotelea kaburini yangehitaji kuondoshwa.
Morison anashangaa kwanini hata maadui wa Yesu waliruhusu “habari ya kaburi tupu” iendelee kama haikuwa kweli. Upatikanaji wa mwili wa Yesu ungezimisha haraka mbinu za ujanja wote.
Na kinachojulikana kihistoria cha maadui wa Yesu ni kwamba waliwashitaki wafuasi wa Yesu kwa kuiba mwili, mashitaka yaliyoashiria wazi imani ya pamoja kwamba kaburi lilikuwa tupu.
Dk. Paul L. Maier, profesa wa historia ya zamani katika Chuo Kikuu cha Michigan Magharibi, vile vile alisema, Ikiwa ushahidi wote unapimwa kwa haki, kwa sana inathibitika kuhitimisha kwamba kaburi ambamo Yesu alikuwa amezikwa kulikuwa tupu asubuhi ya kwanza ya Pasaka. Na hakuna ushahidi wa pamoja uliopatikana bado… ambao ungepinga ukweli huu.”[18]
Viongozi wa kiyahudi walishtushwa, na waliwashitaki wafuasi kuiba mwili wa Yesu. Lakini warumi walikuwa wameweka ulinzi wa saa 24 katika kaburi wa kikosi cha ulinzi kilichofunzwa (kuanzia askari 4 hadi 12). Morison aliuliza, “Jinsi gani wataalamu hawa wangeweza kuruhusu mwili wa Yesu kuharibiwa?” Ingekuwa haiwezekani kwa mtu yeyote kuwa amewaponyoka na walinzi wa kirumi na kuwa amehamisha jiwe la tani mbili. Lakini bado jiwe lilisogezwa mbali na mwili wa Yesu ulikuwa unakosekana.
Ikiwa mwili wa Yesu ulikuwa sehemu yoyote kuonekana, maadui wake wangeuonesha haraka ufufuko wake ni uongo. Tom Anderson, raisi wa zamani wa Chama cha Wanasheria wa California, anaandikwa kwa kifupi uzito wa madai haya:
“Kwa jambo lililotangazwa sana, haufikiri kwamba ni sawa kwa mwanahistoria yeyote, shahidi yeyote, mpinzani yoyote angerekodi kwa muda wote kwamba ameuona mwili wa Yesu?… Ukimya wa historia una nguvu inapokuja kwenye ushahidi dhidi ya ufufuko.”[19]
Kwa hiyo bila mwili wa ushahidi, na kaburi lilijulikana kuwa wazi, Morison alikubali ushahidi ni wa kutosha kwamba mwili wa Yesu ulitoweka kwa namna fulani toka kaburini.