Je, Yesu alikufa?
“Marley alikuwa amekufa kama konokono mlangoni, kwa hilo hakukuwa na shaka” Hivyo ndivyo ulivyoanza wimbo wa Krismas wa Charles Dickens, mtunzi hakutaka mtu yoyote asieleweke vibaya kwa tabia zisizo za kawaida kwa kile kitachotokea muda mfupi baadaye. Kwa namna ile ile, kabla hatujachukua kazi ya CSI na kuunganisha ushahidi wa ufufuko, lazima kwanza tuthibitishe kulikuwa na maiti kwa kweli. Pia katika nyakati fulani magazeti yamekuwa yakiripoti juu ya maiti fulani kwenye chumba cha maiti (mochwari) inayohema na kuamka. Je, ni kitu kama hicho kimetokea kwa Yesu?
Baadhi ya watu wamependelea kusema kwamba Yesu alikuwa hai hata baada ya kusulubiwa na alifufuliwa na hewa ya ubaridi kaburini – “Du, ni kwa muda gani nilikuwa sielewi hili?” Lakini nadharia hiyo haioneshi kuwa na ushahidi wa kitabibu. Makala katika gazeti la chama cha madaktari wa Marekani, inaeleza kwanini hii nadharia iitwayo nadharia dhaifu haikubaliki. “Kwa uwazi kabisa, uzito wa ushahidi wa kihistoria na kidaktari ulionesha Yesu alikuwa amekufa. Mkuki uliochomeshwa katika ya mbavu zake za kulia, yawezekana ulitoboa sio tu pafu lake la kulia, lakini pia ulitoboa ngozi ifunikavyo moyo na moyo wenyewe na hivyo kuhakikisha kifo chake.”[12] Lakini shaka juu ya jambo hili inaweza kuwa katika mpangilio, na suala hili limeachwa hivyo kwa miaka 2,000. Na katika dakika za mwisho, twahitaji maoni mengine ya pili.
Sehemu moja kupata ukweli huo ni katika ripoti za wanahistoria ambao si wakristu toka katika nyakati ambapo Yesu aliishi. Watatu kati ya hawa wanahistoria walitaja kifo cha Yesu.
- Lusiani (c. 120 baadaye 180 A.D. alimkumbukua Yesu kama mwanafalsafa aliyesulubiwa).[13]
- Yosefasi (c. 37 – c 100 A.D.) aliandika, kwa wakati huu alionekana Yesu mtu mwenye busara alikuwa mtendaji wa matendo ya ajabu. Wakati Pilato alipomhukumu msalabani, viongozi miongoni mwetu, walikuwa wamemshitaki, na hao waliompenda hakuwakukoma kufanya hivyo.[14]
- Tasitasi (c. 56 – c. 120 A.D.) aliandika “Kristo, ambaye jina lake lilikuwa na asili yake, aliteseka na kupata adhabu kali mikononi mwa hakimu wetu, Pontio Pilato.”[15]
Hii ni kama kwenda kwenye kumbukumbu na kukuta siku moja ya masika katika karne ya kwanza, Gazeti la Yerusalem liliandika stori kwenye ukurasa wa mbele kwamba Yesu alikuwa amesulubiwa na kufa. Si kazi ngumu ya kipelelezi, na inatupa uhakika mzuri wa hitimisho kuwa Yesu alikuwa amekufa.
Kwa kweli, hakuna maelezo ya kihistoria toka kwa wakristu, warumi, au wayahudi ambayo yanabishia aidha kifo cha Yesu au mazishi yake. Hata Krosani, mkosoaji wa ufufuko, anakubali kwamba Yesu aliishi na alikufa. “Kwamba alisulubiwa ni hakika kwa kilivyo kitu chochote cha kihistoria kinavyoweza kuwa.”[16] Katika kufikiria ushahidi huu, twaonekana kuwa hodari katika nyanja za kuondosha uwezekano wa fikra ya kwanza kati ya zile tano. Yesu kwa hakika alikuwa amekufa, “kwa hilo hakukuwa na shaka”